Tuesday, September 4, 2012

CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA RUVUMA CHATOA TAMKO KULAANI MAUAJI YA MWANAHABARI DAUD MWANGOSI NA KUSITISHA MAHUSIANO NA POLISI

 Mwenyekiti wqa Chama cha Waandishi wa habari Mkoa wa Ruvuma Bw. Andrew Kuchonjoma(wa kwanza kulia) akizungumza na Waandishi wa habari wakati akitoa tamnko.Wa kwanza kushoto ni Katibu wa Chama cha Waandishi wa habari Mkoa wa Ruvuma Bw. Andrew Chatwanga.
 Baadhi ya Wandishi wa habari wa Mkoa wa Ruvuma wakimsikiliza Mwenyekiti wao wakati wa mkutano wao wa kutoa tamko kulaani mauaji ya Mwanahabari Daud Mwangosi yanayodaiwa kufanywa na Jeshi la Polisi.

TAMKO LA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA RUVUMA KULAANI MAUAJI YA MWANAHABARI DAUD MWANGOSI


RUVUMA PRESS CLUB - RPC.
     (CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI RUVUMA)    
               MAWESO Street, TEACHERS’ SACCOS Building Room No.6.
     P.O. Box 1303, Tel: 025 - 2600195, Fax 025 – 2600195
SONGEA, RUVUMA-TANZANIA
Email; ruvumapressclub2@ yahoo.com

SEPTEMBER 04.2012

CHAMA cha waandishi wa habari mkoa wa Ruvuma(RPC)Tunalaani vurugu
zilizotokea juzi mkoani Iringa na kusababisha kifo cha mwandishi wa
habari wa kituo cha utangazaji cha Chanel Ten Daud Mwangosi.ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha waandishi wa Habari Mkoa wa Iringa

jeshi la polisi limekuwa likionyesha wazi wazi kuwa
linatumia nguvu,ubabe na matumizi mabovu ya silaha za moto ambayo
hayajaweza kusaidia siku zote na badala yake kinachoachwa ni maumivu
na vilio kwa wananchi.

Ruvuma press Club kama ilivyo kwa wenzetu wa mikoa yote ya Tanzania Bara Na Visiwani tunasitisha mahusiano na jeshi la polisi kwa muda hadi hapo suala la kuuawa kwa Daudi Mwangosi Mwenyekiti wa Iringa press litakapopatiwa majibu ya kweli na wahusika kuchukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Ruvuma Press club ina wataka viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa kuendesha shughuli zao huku wakijua inawapasa kuangalia na kuwalinda waandishi wa habari wanaokuwa kwenye mikutano yao maana bila ya waandishi kazi zao zinakuwa hazina mafanikio wanayoyapata.

Mwisho tunaitaka Serikali kuunda tume huru itakayotoa majibu sahihi kwa vile kabla ya tume kuundwa tayari tumeona pasipo shaka kupitia picha mbalimbali Daudi Mwangosi akiwa ameshikiliwa na polisi wengi huku akiwa chini na mkono wa kulia ameshika kamera na muda mfupi ikisemekana ameuawa.

Matarajio yetu tume itafanya kazi kwa haki na uwazi na muda mfupi majibu yatatolewa haraka na wahusika watachukuliwa hatua zinazosahili.

Tunarudia kuwaomba vyama vya siasa wanapofanya siasa zao waangalie uhai wa wananchi ,washabiki,wapenzi ,wakereketwa wao na waandishi ambao kimsingi wanakuwa kazini kuripoti mikutano ,maandamano na harakati zote za siasa wajue wanapofanya ubabe wa kutunishiana misuli na wenzao wa jeshi la polisi madhala yanakuwa kwa watu wasio na hatia.

Kwani katika matukio yote ya harakati za vyama vya kisiasa na polisi hatuja shuhudia wanasiasa na polisi  wakiuawa au hata kujeruhiwa badala yake wanaokufa ni watu wasio na hatia na sasa imekuwa mbaya zaidi kwa kuanza kuua waandishi wa habari.

Mwisho tunatoa pole sana kwa wenzetu wa IPC,na familia kwa ujumla tunawaomba wawe na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu mungu awape uvumilivu
amina


Andrew Kuchonjoma
Mwenyekiti Ruvuma Press Club

Nakala
1.Mkuu wa Mkoa Ruvuma
2.Kamanda wa Polisi Mkoa Ruvuma
3.Baraza la habari Tanzania       (MCT)
4.union of Tanzania Press Clubs(UTPC)



 Katibu Mkuu wa Chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Ruvuma Bw. Chatwanga akizungumza kwenye mkutano huo.
 Cresensia Kapinga wa gazeti la Majira akizungumza kwa msisitizo kulaani mauaji ya Bw. Mwangosi.
 Wanahabari wa Mkoa wa Ruvuma wakifuatilia habari ya kifo cha Mwanahabari Daud Mwangosi kwenye magazeti mbalimbali.

 Marehemu Mwangosi(wa kwanza kulia) akizunbgumza wakati wa uhai wake hivi karibuni,wa pili kulia ni Kamadanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa Bw. Michael Kamuhanda.

CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA RUVUMA CHATOA TAMKO KULAANI MAUAJI YA MWANAHABARI  DAUD MWANGOSI NA KUSITISHA MAHUSIANO NA POLISI
Na Julius Konala,Songea.

CHAMA cha waandishi wa Habari mkoani Ruvuma [RPC]kimeungana na vyama  vingine vya waandishi wa habari nchini kulani kitendo cha mauwaji yaliyofanywa na Jeshi la polisi mkoani Iringa katika  vurugu zilizotokea kati ya wafuasi wa chama cha Demokrasia na maendeleo [CHADEMA]na jeshi hilo na kusababisha kifo cha mwandishi wa habari Daud Mwangosi wa wakituo cha chanel Ten mkoani Iringa.

  Tamko hilo limetolewa leo na Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoani Ruvuma Andrew Kuchonjoma wakati akiongea na waandishi wa habari kwenye ofisi ya chama hicho mjini Songea kufuaatia kutokea kwa tukio hilo la kusikitisha .

 Kuchonjoma alisema kuwa kitendo hicho cha mauaji hayo yaliyofanywa dhidi ya mwandishi wa Habari huyo ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa[IPC]kinalaniwa vikali na waandishi wa habari mkoani Ruvuma na kudai kuwa chama hicho kinasitisha mahusiano na Jeshi la polisi kwa muda hadi hapo suala la kuuawa kwa Daud Mwangosi litakapo patiwa majibu ya kweli na wahusika kuchukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

"Jeshi la polisi limekuwa likionyesha waziwazi kuwa linatumia nguvu ,ubabe na matumizi mabaya ya silaha za moto ambayo hayajaweza kusaidia siku zote na badala yake kinachoachwa ni maumivu na vilio kwa wananchi"alisema Kuchonjoma.

"Tunaitaka serikali kuunda tume huru itakayo toa majibu sahihi kwa vile kabla ya tume kuundwa tayari tumeona pasipo shaka kupitia picha mbalimbali Daudi Mwangosi akiwa ameshikiliwa na polisi wengi huku akiwa chini na mkono wa kulia ameshika kamera na muda mfupi akisemekana ameuawa"alisema.

 Aidha Mwenyekiti huyo wa chama cha waandishi habari mkoa wa Ruvuma  amewataka viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa kuendesha shughuli zao huku wakijua inawapasa kuangalia na kuwalinda waandishi wa habari wanaokuwepo kwenye mikutano yao maana bila ya waandishi kazi zao zinakuwa hazina mafanikio.

  Alisema kuwa katika matukio yote ya harakati za vyama vya kisiasa na polisi haijawahi kushuhudiwa kuawa,badala yake wanaokufa ni watu wasio na hatia na kwamba sasa imekuwa mbaya zaidi kwa kuanza kuua waandishi wa habari.

              MWISHO.

  

 Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa Bw. Michael Kamuhanda.
 Marehemu Mwangosi akisisitiza jambo wakati wa uhai wake.
Marehemu Mwangosi(wa kwanza kulia,walioketi)akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Mkoaa wa Iringa enzi za uhai wake.Marehemu Mwangosi alikuwa Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa habari Mkoa wa Iringa(IPC) NA Mwakilishi wa Kituo cha Chenel Ten Iringa.

No comments:

Post a Comment