Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Mkoani Njombe Bw. George Mkindo.
WANANCHI KATIKA MJI WA NJOMBE WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA
MAENDELEO
Na Joseph Mwambije
Njombe
WANANCHI katika
Halmashauri ya mji wa Njombe Mkoani Njombe wametakiwa kuchangamkia fursa za kibiashara na kimaendeleo zilizopo katika mji huo ili waweze kujiletea
maendeleo na kuupaisha kimaendeleo Mkoa
huo mpya.
Hayo yameelezwa juzi na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa
Njombe Bw. George Mkindo wakati
akizungumza na Mtandao huu Ofisini kwake Mjini Njombe kuhusiana na mikakati mbalimbali ya
maendeleo ya Halmashauri hiyo.
Anasema Halmashauri
hiyo ina fursa nyingi za maendeleo katika upandaji wa miti ya kutengeneza
madawa ya kulainishia ngozi za viatu ambayo anasema pia imekuwa ikiuzwa Ulaya na
Nchi nyingine za Afrika.
Anataja fursa nyingine zilizopo ambazo zinapaswa kuchangamkiwa
na wananchi ni za ufugaji wa samaki na nyuki
na kilimo cha maua ambacho kinastawi vizuri katika mji huo na kumekuwa na Wawekezaji
wawili wa kizungu wanaendesha kilimo hicho.
‘Mji wa Njombe una fursa nyingi za kimaendeleo ambazo kama wakizitumia vyema wataondokana na
umaskini,kwa mfano tuna kilimo cha maua
kinachostawi vizuri ambacho kinaendeshwa na Wawekezaji wawili wa
Kizungu’anasema Mkurugenzi huyo.
Mkurugenzi huyo anasema kuwa wana viwanda vitatu ambavyo ni
Kiwanda cha miti cha TANWAT,Kiwanda cha
chai Luponde,Kiwanda cha kusindika
maziwa na Viwanda vingine vidogovidogo.
Hata hivyo anasema wanakabiliwa na changamoto mbalimbali
zinazokwaza uendeshaji wa Halmashauri hiyo kama pesa za maendeleo kutowafikia
kwa wakati na upungufu wa watumishi
katika Idara zake.
Mwsho
No comments:
Post a Comment