HABARI KAMILI
WATU wanane wameuawa na wengine kumi na moja
kujeruhiwa kutokana na vurugu zilizizotokea jana mkoani Mtwara na Itete
wilayani Ulanga, mkoani Mororgoro.
Muuguzi wa zamu katika Hospitali ya Wilaya ya
Masasi, Mkomaindo, Amima Simbo alithibitisha vifo vya watu saba
waliofikishwa hospitalini hapo.
Kwa mujibu wa muuguzi huyo, maiti zilizopokelewa
hospitalini hapo zilionekana zikiwa na matundu yanayodhaniwa kuwa ni ya
risasi, baadhi yao kichwani, begani, viunoni na tumboni.
Aidha majeruhi waliofikishwa hospitalini hapo pia walikuwa na majeraha mbalimbali ikiwamo ya risari.
Aidha majeruhi waliofikishwa hospitalini hapo pia walikuwa na majeraha mbalimbali ikiwamo ya risari.
Habari zaidi zinaeleza kuwa vurugu hizo zilizuka
baada ya kundi la waandamaji, wengi wakiwa vijana waendesha pikipiki
maarufu kama bodaboda waliokuwa wakipinga mwenzao kukamatwa na kutaka
kuvamia Kituo cha Polisi ili kumwokoa.
Vurugu hizo ziliendelea kuutikisa Mkoa wa Mtwara
kwa siku ya pili mfululizo na kuutikisa Mkoa wa Mtwara, baada ya vurugu
nyingine kuibuka wilayani Masasi jana.
Habari zinasema mbali na vifo na majeruhi, nyumba
za wabunge wawili wa wilaya hiyo zimechomwa moto, ambapo pia magari,
trekta, Ofisi za CCM Wilaya na Ofisi ya Mkurugenzi wa Wilaya
ziliharibiwa kwa kuchomwa moto.
Wabunge ambao nyumba zao zimemwa moto ni Mariam Kasembe wa Masasi Mjini na Anna Abdallah Mbunge wa Viti Maalumu wilayani humo.
Juzi vurugu hizo zilitokea katika Mikoa ya
Morogoro kati ya wakulima na wafugaji na kusababisha kifo cha mtu mmoja
wakati mkoani Mtwara wananchi wa eneo la Chikongola waliizingira nyumba
ya diwani wa Kata ya Mikindani, Mohamedi Chehako kwa madai ya
kuwahifadhi wachawi ndani ya nyumba yake.
Katika vurugu hizo polisi walilazimika kutumia
silaha yakiwamo mabomu ya machozi ili kupoza hali ya hewa, ambapo nyumba
ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa (Tamisemi), Hawa Ghasia ilichomwa moto.
Akizungumza na Mtandao huu kuhusu vurugu
hizo, Mbunge wa Masasi Mjini, Mariam Kasembe alisema kuwa nyumba yake
iliyoko Masasi mjini imechomwa moto na kuteketea kabisa, huku mali
zikiibwa na kwamba familia yake sasa haina makazi.
Aliongeza kwamba mbali na uharibifu, vurugu hizo zimesababisha pia mama yake mzazi kukimbia na mpaka sasa hajulikani alipo.
“Wamechoma trekta na gari lililokuwepo nyumbani
kwangu, watoto wangu na mume wangu walipoona hali hiyo wakakimbia,”
alisema Kasembe akieleza kuwa hawezi kuthibitisha chanzo cha vurugu
hizo, lakini anahisi kuwa zinatokana na mgogoro wa gesi.
CHANZO-GAZETI LA MWANANCHI
CHANZO-GAZETI LA MWANANCHI
No comments:
Post a Comment