Saturday, November 10, 2012

SHIRIKA LA WATAWA WABENEDIKTINE LA PERAMIHO SONGEA LAKANUSHA KUHUSIKA NA MAUAJI YA PROFESA MWAIKUSA

 .Ni baada ya gazeti moja la wiki kulihusha na mauaji

Na  Joseph Mwambije
Songea
SHIRIKA la Watawa Wabenediktine la  Peramiho Mkoani Ruvuma  ambalo liko chini ya Kanisa Katoliki limekanusha habari zilizochapishwa na gazeti moja la wiki likilihusisha na  mauaji  ya  Mhadhiri wa Chuo kikuu  cha Daressalaam kitivo cha Sheria  Marehemu Profesa Jwan Mwaikusa aliyeuawa kwa kupigwa risasi mwaka Julai 13 mwaka 2010.

Akizungumza na Waandishi wa habari Ofisini kwake Peramiho Songea Mkoani Ruvuma Makamu Mkuu  wa Shirika hilo ambaye pia ni Mtawa wa Shirika hilo,Fidelis Mligo  anasema kuwa  ameshtushwa na taarifa hizo alizodai kuwa ni za uzushi na hazina ukweli wowote na zina lengo la kulichafua Shirika hilo la kidini.

Kiongozi huyo anasema kuwa hamfahamu  Marehemu   Profesa Mwaikusa na hajawahi kumuona  na kwamba   aliyewahi kuwa Mtawa wa Shirika hilo ambaye aliwahi kutiwa hatiani Januri 2012 na Mahakama ya Hakimu Mkazi Songea kwa kosa la kuiliibia Shirika hilo Bw. Nestory Muhuwa(Br Aidan)  na ndiye anayemjua.


Ni Kiongozi Mkuu(Abate) wa Watawa Wabenediktine wa Peramiho Mtawa Anastasius Reiser  OSB

Alidai kuwa    shirika hilo linapakwa matope na baadhi ya watu wenyenia mbaya kwa maslahi yao binafsi na kusahau kuwa shirika siyo la mtu mmoja bali ni taasisi inayotengemewa na jamii kwa utoaji huduma zinazo stahili.
 
Akielezea kuhusiana na Abasia hiyo kuwa wanahisa kwenye kampuni ya uchimbaji wa madini  ya UMICO   ya Lukarasi Wilayani Mbinga alisema kuwa tangia mwaka 1990 walikuwa wamejiunga kuwa wanahisa na msimamizi mkuu alikuwa Bw.Nestory Mhuwa [Br Aidan]na baadae shirika hilo lilijitoa kutokana na usimizi mbovu wa  Mtawa huyo  ambaye  alifukuzwa utawa kutokana  na makosa mbalimbali.

“Shirika hili siyo la mtu binafsi bali ni taasisi inayofanyakazi kwa taratibu na kanuni kwa mjibu wa sheria zilizo wekwa tofauti na baadhi ya watu wanavyofikiria ,kwa kufanya mipango ya kupaka matope na kutaka kukwamisha shughuli zinazofanywa na shirika hilo mbele za jamii”alisema  Kiongozi huyo.

Anabainisha kuwa Shirika hilo halikupanga mauaji hayo na kwamba hakukuwa na ugomvi wa kugombea umiliki wa mgodi wa dhahabu wa Lukarasi ulioko Wilayani Mbinga Mkoani Ruvuma na kwamba wao hawakuwa  wamiliki wa mgodi huo bali walikuwa Wanahisa kabla ya kujitoa mwaka 2010.

Mtawa huyo  anafafanua kuwa taarifa zilizochapishwa kwenye gazeti ni za kupikwa na kwa mujibu wa Sheria ya Kanisa Katoliki Mtawa haruhusiwi kuwa na mali binafsi na hivyo umiliki wa hisa katika mgodi huo haukuwa wa siri.
Mwisho

1 comment:

  1. haya magazeti inabidi kabla ya kuandika habari nzito kama hizi yafanye kwanza utafiti wa habari husika

    ReplyDelete