Mkapa akifukiziwa uvumba pamoja na Viongozi wengine wa Mkoa wa Ruvuma kwenye Kanisa la Mtakatifu Kilian Mbinga Mkoani Ruvuma kwenye jubilei ya miaka 25 ya Jimbo la Mbinga na miaka 25 ya utumishi wa Askofu msfaafu wa Jimbo hilo Mhashamu Emannuel Mapunda.
Baaadhi ya Maaskofu wakiongozwa na Askofu Mku wa Jimbola Songea Askofu Mkuu Norbert Mtega wa (pili kulia) wakiwa kwenye Sala katika jubilei hiyo
Balozi wa Papa hapa Nchini naye alikuwepo,hapa anatoa Neno.
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Bw. Benjamin Mkapa akiwa na Mkewe Anna Mkapa wakifuatilia kwa makini mafundisho Kanisani hapo.
Rais Mstaafu Mkapa ambaye pia alikuwa mgeni Rasmi akizungumza Kanisani hapo ambapo aliwataka wananchi kutumia haki yao ya kimsingi kujitokeza kutoa maoni yao kwenye mikutano ya kukusanya maoni8 ya kupatikana kwa Katiba mpya,.
Hapa anahutubia.
I AM FREE LANCER JOURNALIST IN SONGEA,RUVUMA REGION 0755761195,0655761195 josephmwambije@yahoo.co.uk josephmwambije@gmail.com
Monday, July 30, 2012
WALIMU RUVUMA WAGOMA,KAIMU RC AHAHA KUZIMA MGOMO BILA MAFANIKIO
Na Joseph Mwambije
RUVUMA
WALIMU katika
Shule mbalimbali Mkoani Ruvuma wameendelea na mgomo wao usiokuwa na
kikomo kuishinikiza Serikali kushughulikia madai yao huku Kaimu Mkuu wa
Mkoa huo Joseph Mkilikiti akitishia kuwafukuza kazi walimu
waliogoma ambapo katika Shule nyingine walimu hawakufika kabisa Shuleni
hali iliyofanya wanafunzi kurejea nyumbani.
Mwandishi
wa habari hizi alitembelea Shule mbalimbali za Manispaa ya Songea na
kushuhudia walimu wakiwa kwenye mgomo huku baadhi ya Shule walimu
wakifika kuripoti na kurejea nyumbani.Huku katika Shule nyingine walimu
walionekana wakiota moto na kusema hawafundishi wanaota moto.
Baadhi
ya Shule ambazo walimu wake wamegoma ni Shule za Msingi
Sabasaba,Mwembechai,Makambi,Mahilo,Majimaji,Sokoine,Bombambili,Sabasaba,Matarawe,Makambi
na baadhi ya Shule za Sekondari huku katika Shule mbili za Manispaa ya
Songea walimu wakiendelea na kazi hali iliyofanya Viongozi wa Chama cha
walimu kuwazuia kufanya kazi.
Katika Shule ya
Msingi Matarawe Mwandishi alishuhudia ikiwa na walimu watatu akiwemo
Mwalimu Mkuu ambapo walisema wao wamebaki kutokana na mradi wa Shule wa
kuuza uji kwa wanafunzi vinginevyo wangekuwa wamerejea nyumbani.
Katika
Shule ya Msingi Matarawe yenye walimu 16 ni walimu watatu pekee ndio
walikuwepo Shuleni hapo akiwemo Mawalimu Mkuu wa Shule hiyo aliyeomba
jina lake lisiandikwe gazetini ambaye alisema Kaimu Mkuu wa Mkoa huo,
Mkilikiti amekuwa akizunguka kuwatishia kuwafukuza kazi walimu
waliogoma.
Katika hatua nyingine Kaimu Mkuu
huyo wa Mkoa amewaagiza Watendaji wa Kata kuorodhesha
majina ya walimu waligoma ambapo Mwandishi wa habari hizi alishudia
baadhi ya Watendaji wa Kata wakiorodhesha majina ya walimu waliofika
kuripoti Shuleni na kuendelea na mgomo na waliogoma kabisa hata kuja
Shuleni.
Gazeti hli lilipotembelea kwenye Ofisi
za Chama cha walimu Mkoa wa Ruvuma lilishuhudia viongozi wa Matawi ya
vyama vya walimu toka kwenye Shule 72 za Manispaa ya Songea wakiwa
kwenye majadiliano ya kupeana misimamo zaidi ya kuendelea na mgomo huo
usiokuwa na kikomo hadi Serikali itakaposhughulikia madai ya walimu.
Baadhi
ya Viongozi wa Chama cha walimu Mkoani humo ambao hawakupenda majina
yao yaandikwe gazetini wakizungumzia hatua ya Kaimu Mkuu wa Mkoa ya
kuwatisha walimu waliogoma walisema hakupaswa kufanya hivyo kwa kuwa
mgomo huo uko kihalali.
Hata hivyo Kaimu Mkuu
wa Mkoa wa Ruvuma ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Songea alipozungumza
na
gazeti hili kwa njia ya simu kuhusiana na mgomo huo alisema wana vikao
viwili kujadili suala la hilo na bado wanalifuatilia na atakapomaliza
vikao hivyo atakuwa na maelezo kamili.
Alipoulizwa
kuhusu madai ya kuwatisha kuwafukuza kazi walimu waliogoma alikana
kufanya hivyo na kusema yeye alitembelea kujionea hali halisi ya mgomo
ambapo alimwambia Mwandishi wa habari hizi awasiliane na Meya wa
Manispaa ya Songea, Charles Mhagama.
Kwa
upande wake Meya wa Manispaa ya Songea alipozungumza na gazeti hili kwa
njia ya simu alisema hali ni mbaya kuhusiana na mgomo huo ambsapo
anasema walipotembelea yeye na Mkuu wa Wilaya walishuhudia kukiwa na
walimu wachache huku katika Shule nyingine kukiwa hakuna walimu kabisa.
'Wengine
walikuja kuripoti na kurudi nyumbani huku wengine wamegoma kabisa hata
kuja Shuleni ni kweli tumeagiza Watendaji wa Kata waorodheshe idadi ya
walimu wealiogoma ili tujionee hali halisi na Serikali ijue hatua za
kuchukua'alisema.
Alipoulizwa
malalamiko ya walimu waliogoma kutishwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa kuwatisha
walimu kuwafukuza kazi alisema hakuwatisha bali aliwaambia kuwa
watafukuzwa kazi na kusisitiza kwamba walimu watakaogoma watachukuilwa
hatua na Serikali ikiwa ni pamoja na kufukuzwa kazi.
Aliwatoa
wito kwa walimu kuachana na mgomo na kuendelea na kazi na kuwataka
kuachana na maneno ya watu wanaowashawishi kugoma kwa kuwa wakifanya
hivyo hatua dhidi yao zitachukuliwa.
Madai ya msingi ya Walimu ni nyongeza ya mshahara na posho ya kufundisha katika mazingira magumu
Wanafunzi wakicheza baada ya walimu wao kugoma
Kibao cha Shule ya Msingi Mfaranyaki ambayo walimu wao waliendelea na mgomo ambapo ikalazimu Viongozi wa Chama cha walimu kwenda kuwazuia kufanya kazi.
Jengo la Chama cha walimu Mkoa wa Ruvuma ambako ndiko ziliko ofisi za Chama cha Walimu Mkoa huo na Wilaya zake.
Walimu wakiendelea na majadiliano ya kuendelea na mgomo wao usio kuwa na kikomo hadi Serikali itakaposhughulikia madai yao.
Wednesday, July 25, 2012
SIMBA YAPATA KIPIGO CHA MBWA MWIZI MSITU WA PANDE
Kitendo kama hicho cha kinyama ndicho kinachofananishwa na ilichofanyiwa Simba jana na mshambuliaji wa Azam, John Boko baada ya kufunga mabao matatu pekee na kuiwezesha timu yake kushinda 3-1 katika mechi ya robo fainali ya Kombe la Kagame kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Kwa ushindi huo sasa Azam itacheza mechi ya nusu fainali ya Kombe la Kagame dhidi ya AS Vita ya DR Congo iliyoitoa Atletico ya Burundi kwa mabao 2-1 katika mechi iliyochezwa awali. Boko alifunga bao lake la kwanza dakika 17, akiunganisha kwa kichwa krosi ya Ibrahimu Shikanda, kisha akapachika la pili kwa shuti dakika 46 akimalizia pasi ya Kipre Tchetche, kabla ya Shomari Kapombe kuifuta machozi Simba dakika 53, lakini Boko mfungaji bora wa msimu uliopita alizima ndoto za Simba kurudi kwa kupachika bao la tatu kwa shuti la chini lililomshinda Juma Kaseja na kujaa wavuni. Katika kile kinachoonekana kujaa kwa imani za kishirikina jana klabu za Simba na Azam hazikutumia mlango mkuu wa kuingilia uwanjani baada ya kumaliza kufanya mazoezi. Simba wenyewe walitokea geti la kaskazini na Azam walipita mlango tofauti wakati wakirejea vyumbani tayari kujiandaa na mechi hiyo. Simba ilianza mchezo huo kwa kasi na kufanikiwa kufika langoni kwa Azam katika dakika ya kwanza na saba, lakini Haruna Moshi na Felix Sunzu na Uhuru Selemani walishindwa kutumia nafasi hizo. Katika mechi hiyo Sunzu alipewa kadi ya njano na mwamuzi Issa Kangabo kutoka Rwanda kwa kumchezea vibaya Tchechte. Mwanzoni mwa kipindi cha kwanza Uhuru Selemani alipoteza nafasi mbili za kufunga baada ya kuwatoka mabeki wa Azam, lakini jitihada zake ziliishia mikononi mwa kipa Deogratius Munishi, huku Azam wakijibu mapigo dakika 14 baada ya Kipre kuwatoka mabeki wa Simba na kupitisha pasi kwa Hamis Mcha aliyepiga fyongo shuti lake. Dakika ya 17 beki Shikanda wa Azam alipokea pasi ndefu kutoka katikati ya uwanja na kupiga krosi iliyotua kichwani kwa Bocco ambaye alipiga kichwa kilichokwenda wavuni na kumwacha Kaseja akiwa amesimama. Simba walijaribu kurudi mchezoni, lakini mashuti ya Kapombe na Mwinyi Kazimoto dakika 34 na 36 yalishindwa kulenga goli. Dakika 41 mwamuzi aliinyima Simba penalti baada ya Kazimoto kumuangusha Ramadhan Chombo kwenye eneo la hatari. Azam walianza kipindi cha pili kwa kasi na kufanikiwa kupata bao la pili dakika 46 kupitia Boko aliyemalizia vizuri kazi ya Tchetche aliyekuwa mwiba kwa ngome ya Simba. Mchezaji bora wa mwaka wa Taswa, Kapombe aliifungia Simba bao dakika 53 akipokea krosi ya Haruna Shamte na kupiga shuti kali akiwa ndani ya 18 lililomshinda Munishi. Kocha wa Azam, Stewart Hall aliwapumzisha Tchetche, Mcha na kuwaingiza George Odhiambo na Jabir Aziz, wakati Simba ilimtoa Uhuru, Jonas Mkude, Mudde Musa na kuwaingiza Kigi Makasi, Amri Kiemba na Hamis Kinje. Mabadiliko hayo yalionekana kuwa na faida kwa Azam kwani dakika 73, Aziz alitoa pasi kwa Boko na kupiga shuti la chini akiwa nje ya 18 na kwenda moja kwa moja wavuni na kuwanyamazisha kabisa mashabiki wa Simba. Awali Atletico ya Burundi inayosifiwa kwa kucheza soka ya kuvutia iliyaaga mashindano hayo kwa kuchapwa mabao 2-1 na AS Vita ya DR Congo. Mshambuliaji Etekiama Taddy alifunga bao lake la sita kwenye michuano hiyo alipozifumania nyavu za Atletico katika dakika ya 8 na kuifanya AS Vita kumaliza kipindi cha kwanza wakiwa mbele kwa bao 1-0. Atletico ilirudi vizuri na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha dakika 48 kwa shuti kali lililopigwa naPierre Kwizera akiitumia vizuri pasi iliyopigwa na Henry Mbazumutima. Wakati mashabiki wakidhani mpira huo utaamuliwa kwa mikwaju ya penalti, mshambuliaji Basilua Makola aliifungia AS Vita bao la ushindi katika dakika za nyongeza na kufanya mchezo huo kumalizika kwa 2-1. Nusu fainali ya michuano hiyo itaendelea tena kesho kwa Azam kuivaa AS Vita saa nane mchana na mabingwa watetezi Yanga kupepetana na APR saa kumi jioni kwenye Uwanja wa Taifa. |
WANASAYANSI-UKIMWI SIYO TISHIO TENA DUNIANI
WASEMA SILAHA ZOTE ZA KUKABILI VVU WANAZO, WAOMBA FEDHA WAINGIE KAZINI
WANASAYANSI
mbalimbali wanaoendesha tafiti mbalimbali za kutafuta tiba na chanjo ya
Ukimwi, wameitangazia dunia kuwa hatua waliyofikia sasa wanauona
ugonjwa huo ‘siyo hatari tena’ kwa sababu wanazo silaha zote za kuweza
kukabiliana nao.
Ila wakasema,
kinachowakwamisha ni ukosefu wa fedha ambazo zinahitajika katika
kuendeleza tafiti na kuweka sera mpya za kukabili Virusi Vya Ukimwi
(VVU) duniani.
Hayo yalibainika kwenye siku ya
pili ya Mkutano wa 19 wa Kimataifa wa Ukimwi unaofanyika mjini
Washington DC, Marekani na unahudhuriwa na watu zaidi 22,000 miongoni
mwao wakiwamo wataalamu wa afya, watunga sera na wadau wa mapambano
dhidi ya ugonjwa huo toka karibu kila kona ya dunia.
Kwa
mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Kitengo cha
Habari cha Mkutano huo na gazeti hili kufanikiwa kupata nakala yake,
ilieleza kwamba jopo la wanasayansi nguli duniani walikiri kuwa
wamefanyia VVU utafiti wa kutosha ndiyo maana wanatamba kuwa
wamefanikiwa katika kuvidhibiti.
“Kwa sasa
tunazo silaha zote za kisayansi kumalizia mbali gonjwa hili la Ukimwi.
Kilichobaki ni kutumia kikamilifu utaalamu huu katika fursa hii tuliyo
nayo,” alisema Rais wa Taasisi ya Kijamii ya Kimataifa ya Mapambano
dhidi ya VVU (IAS), Dk Elly Katabira.
Kiongozi
huyo ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa Mkutano huo akitokea nchini Uganda,
aliongeza: “Kufanikisha hilo ni lazima tukubali kubadili mfumo kwa maana
kwamba kuweka sera mpya zitakazowezesha kuokoa kundi linaloathirika
zaidi na ugonjwa huu.”
Dk Katabira alifafanua:
“Kinachohitajika ni kuweka mfumo utakaowashirikisha wafadhili na watunga
sera katika kuweka mpango mzuri wa pamoja tuweza kulimaliza tatizo kwa
silaha hizi za kisayansi.”
Naye Mtaalamu wa
Tiba katika Chuo Kikuu cha California, Profesa Diane Havlir alisema:
“Ujumbe wangu kwenu, hasa kwa watunga sera ni kwamba: endeleeni kuwekeza
katika mipango ya kisayansi.”
Kwenye mkutano
huo walishiriki pia wanasayansi wenye dawa na ushahidi unaoonyesha kuwa
katika miaka ya karibuni zimeonyesha dalili nzuri za kutibu Ukimwi na
kifua kikuu (TB).
Wataalamu wengi wa afya
waliunga mkono kauli hiyo wakisema kwa sasa kuna uelewa mkubwa wa
kitaalamu juu ya muundo na tabia ya VVU hivyo ni rahisi kwao kutengeneza
dawa kwa ajili ya kuzuia, kutibu na chanjo.
Tafiti za awali
Kauli
ya wanasayansi hao imekuja baada ya miaka 30 ya kipindi kigumu cha
kutafiti namna ya kupata chanjo au tiba ya ugonjwa huo ambao umeua
mamilioni ya watu duniani, hususan wataalamu na nguvu kazi inayohitajika
kuimarisha uchumi.
Waligundua VVU mwaka 1981
na ilikuwa vigumu kupata dawa ya kuviua kwa sababu ya tabia zao na uwezo
wa kujigeuza kuwa sehemu ya mwili na kutumia selikinga kuzalisha virusi
wengine.
Wanasayansi hao walitoa kauli hizo za
matumaini kukabili VVU mbele ya viongozi mashuhuri wa kisiasa, akiwemo
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Hillary Clinton na Rais wa Ufaransa,
François Hollande.
Mtaalamu anayesimamia
mipango ya afya Ikulu ya Marekani, Profesa Antony Fauci, ambaye piya ni
Mkurugezi wa taasisi ya nchi hiyo ya Utafiti wa Magonjwa ya Kuambukiza
na Mzio (NIAID), alikuwa miongoni mwa waliohutubia na kusifu hatua
iliyofikiwa na wanasayansi duniani.
Ofisa Mkuu
na Rais wa Taasisi ya Mapambano ya Ukimwi nchini Marekani, Phill Wilson
aliweka bayana kuwa pamoja na ugonjwa huo kuonekana tishio hasa kwa
nchi zinazoendelea, hakuna nchi, hata zile tajiri, ambazo zinaweza
kutamba haziathiriki na tatizo hilo.
Kwa hivyo
akasema mikakati na sera mpya za kisayansi zinahitajika dunia nzima,
hivyo akawataka wanasayansi hao ‘kuanika hadharani silaha zao’ ili
zianze kutumika ulimwenguni kote.
Mkurugenzi wa
Shirika la Umoja wa Mataifa wa Mapambano ya Ukimwi (UNAIDS), Sheila
Tlou aliwataka wataalamu hao kuweka mkakati mzuri utakaowezesha silaha
hizo za kisayansi kuelekezwa katika nchi maskini hasa barani Afrika.
Wanasayansi
hao wamekuja na kauli hizo za matumaini wakati ambapo tayari wamefanya
tafiti mbalimbali na kugundua tabia za VVU ikiwa ni pamoja na vitu
ambavyo vinaviwezesha kushambulia seli nyeupe za damu, maarufu kwa jina
la CD4, ambazo ni sehemu ya kinga ya mwili wa binadamu.
Licha
ya tafiti mbalimbali kuonyesha kuwa kuna kila dalili ya kupatikana kwa
chanjo, miaka michache iliyopita, waligundua moja ya dawa zinazotumika
kupunguza makali ya VVU (ARV) ijulikanayo kama Truvada, yenye uwezo wa
kumkinga mwathirika kumwambukiza mpenzi wanayeshiriki naye tendo la
ndoa.
Wiki chache zilizopita, Mamlaka ya
Chakula na Dawa ya Marekani (FDA) iliidhinisha Truvada, ambayo ilianza
kutumika sehemu mbalimbali duniani tangu mwaka 2004, kuwa ni tiba ya
kuzuia kuenea kwa Virusi Vya Ukimwi (VVU).
Kwa
mujibu wa maelezo ya FDA, mwathirika anayetumia dawa hiyo anaweza
kujamiiana na mwenza wake ambaye hana VVU bila kutumia kondomu na
hatomwambukiza.
Matokeo ya utafiti huo wa ARV
yaliwahi kuchapishwa kwenye gazeti hili toleo la Februari 12, mwaka huu.
Kwa mujibu wa FDA, Truvada inatarajia kuanza kutumika na kusambazwa
duniani katika kipindi cha miezi mitatu ijayo.
|
KUNA UKWELI GANI KUHUSU MWISHO WA DUNIA?
NA JOSEPH MWAMBIJE
KATIKA
miaka ya hivi karibuni watu wamekuwa wakiishi kwa hofu kutokana na
tabia za watu mbalimbali ambao wamekuwa wakitabiri kuhusiana na mwisho
wa dunia na kwamba Sayansi ya Dunia iko ukingoni.
Tabiri
hizi zimekuwa zikiweka watu njia panda ambapo wengine wamekuwa
wakitafakari ikiwa Yesu au Issa bin Mariam atakuja watajibu nini ilhali
hawana maandalizi yoyote lakini wengine wenye mioyo dhaifu wanadiriki
kuacha shughuli zao na kumsubiri Yesu huku wengine wakienda milimani
kusubiri ujio wake.
Mwaka
jana tulishuhudia vituko zaidi vya vikundi vya watu waliowaachisha
watoto wao shule na kwenda milimani kusubiri ujio wa Bwana Yesu na
wengine wakitaka kwenda Ulaya kuhubiri injili bila kuwa na paspoti na
tiketi za Ndege kwa madai kuwa mwisho wa dunia umefika.
Lakini
taarifa za hivi karibuni ambazo zimedai kuwa ifikapo Disemba 21 mwaka
2012 ni mwisho wa dunia zimezua hofu zaidi kwa wakazi wa dunia, hofu
inatanda zaidi kutokana na kauli za Wanasayansi wanaodai kuwa Sayari ya
dunia hii imebakiza miezi michache kufikia ukomo wake.
Kauli
za Wanasayansi hao zinasimamia kwenye vipimo vya tabiri za mnajimu wa
Kifaransa, Michael de Nastredame aliyeishi karne ya 16 (1503 – 1566), tabiri
za mnajimu huyo maarufu kupitia kitabu chake cha Les Prophetics
(Ubashiri) zinadai kuwa mwaka 2012 kutakuwa na vita ya tatu ya dunia
itakayosababisha maangamizi makubwa ya dunia.
Kutokana
na utabiri huo Wanasayansi walio katika mlengo wa kat ya Sayansi na
Unajimu wanayajengea hoja maandishi ya Nostradumus kuwa uwepo wa Nishati
za Nyuklia katika Nchi mbalimbali ndiyo zao la dunia wakati wa Vita Kuu
ya tatu. Kwa wale wanaofuatilia makala zangu kuna wakati niliwahi
kuandika Makala yenye kichwa, Mzozo wa Israel na Irani na hofu ya kuzuka
Vita ya tatu ya dunia.
Baadhi
ya Nchi zinazomiliki Nishati ya Nyuklia ni Marekani, baadhi ya Nchi
zilizokuwa zinaunda Umoja wa Soviet , China , Ufaransa , India ,
Pakistan , Iran na Korea Kaskazini. Athari za
mabomu ya Nyuklia zipo Hiroshima Nchini Japan ambapo athari zake zipo
hadi leo kutokana na bomu hilo la Atomic lililotupwa wakati wa Vita ya
Pili ya dunia mwaka 1939 hadi
mwaka 1945.
Kutokana
na makali ya Bomu hilo ambalo liliua watu 80,000 na wengine wengi
kujeruhiwa Japan ilisalimu amri na vita hiyo ikakomeshwa, katika Mji wa
Hiroshima ambako lilitupwa bomu hilo hadi leo bado watu wanazaliwa
vilema huku kukiwa na simanzi isiyofutika. Nchi za Israel , Afrika
Kusini , Argentina na Brazil zinatajwa kuwa na uwezo wa kumiliki na
kutumia Nyuklia lakini bado hazina mpango wa kumiliki na kurutubisha
silaha hizo za maangamizi.
Wanasayansi
wanaeleza kuwa kizaazaa cha dunia kuangamia ni tufani zito ambalo
litaigonga na kusababisha kupoteza mawasiliano kati yake na jua hivyo
ile sumaku ya asili kushindwa kufanya kazi yake, katika maelezo yao
wanasayansi wanafafanua kuwa kuna Sayansi inayoitwa Nibiru Planet x
ambayo itapoteza mwelekeo Disemba 21 2012na kuigonga dunia na
kusababisha itoweke.
“Hii
ina maana kuwa baada ya Disemba 21, 2012 hakutakuwa na Sayansi
inayoitwa dunia kwani itagongwa na Planet x na kuipoteza, itaiachanisha
na jua kisha itadondoka” ilisema sehemu ya ripoti ya Wanasayansi hao.
Hata hivyo kwa upande wa pili Wanasayansi wa Taasisi ya NASA ya Nchini Marekani wanautaka Ulimwengu kutambua kwamba 2012 si mwisho wa dunia huku wakiwataka wakazi wa
dunia kutokuwa na wasiwasi kuhusiana na habari za mwisho wa dunia. NASA
wanadai kuwa katika matoleo yote yanayoelezea kuwa dunia mwisho wake ni
2012, hakuna hata moja ambalo wamejiridhisha kitaalamu badala yake
wameelezea hali hiyo kwamba inakuja kwa lengo la kutisha watu.
Habari
za mwisho wa dunia hazijaanza leo ambapo iliwahi kuelezwa kuwa mwaka
1844 ni mwisho wa dunia, pia ikaelezwa kuwa mwaka 2000 ni mwisho wa
dunia lakini pia ikavumishwa kuwa mwaka 2003 ndio ingekuwa ukomo wa
dunia. Pia kumekuwa na watu wengi ambao wamekuwa wakiibuka na
kujitangaza kuwa wao ni Yesu.
Lakini
hebu twende kwenye hoja za msingi katika biblia na vitabu vingine vya
dini tuone ukweli uko wapi, madai hayo ya mwisho wa dunia yana ukweli
gani? Je Biblia inawaitaje wanazusha kuhusu mwisho wa dunia na kwamba
matukio yanayotendeka sasa yanaashiria nini?
Hofu
imetanda huku baadhi ya maeneo wakishindwa hata kufanya kazi
wakijiandaa na mwisho wa dunia, kwingineko duniani wameuza walivyonavyo
na kusaidia maskini kisha kubaki watupu wakisubiri ujio wa Yesu kwa hofu
kuu wakiwa na hoja kwamba mali wanazomiliki hazina maana wakati dunia
imefika mwisho, lakini pia ndani ya biblia tutaona kama hayo ni maagizo
ya Yesu.
Watu
waishi kwa hofu wakihofia mwisho wa dunia, pia tutaona kama kuna
tarehe, mwezi na mwaka vilivyotajwa kuwa ni mwisho wa dunia na Ujio wa
Yesu? Naam kwa wale wasiyoyafahamu Maandiko Matakatifu.wanakuwa na hofu
kubwa hadi kufikia kiwango cha kupatwa shinikizo la damu au ugonjwa wa
moyo wakihofia mwisho wa dunia.
Katika hofu zao ndipo na matapeli wanawajia wakidai wakidai wao ni akina Yesu na Manabii waliotumwa na Mungu kuja
kuwapa maonyo na kuwataka kukabidhi mali zao kwa akina Yesu hao na
Manabii hao wa Uongo. Katika miaka ya hivi karibuni tumeshuhudia akina
Yesu wengi wa uongo na Manabii wa uongo.
Dunia
bado haijasahau yale yaliyotendwa na Nabii wa uongo Bw. Kibwetere na
kule Uganda aliyewaamuru wafuasi wake wamkabidhi mali zake na kusubiri
mwisho wa dunia wakiwa kanisani, mwisho uliowajia kwa Nabii huyo wa
uongo kuwachoma moto wakiwa kanisani na familia zao.
Mikanganyiko
hii itazidi kuwaathiri wengi wasioyafahamu maandiko kadri tunavyosonga
mbele huku akina Yesu wa bandia wakizidi kuibuka na kutoa mafundisho
kinyume na Yesu wa ukweli ambaye kwa mujibu wa Biblia yuko mbinguni
akiwaombea watu wake pengine hili suala la mwisho wa dunia au kiama ni
suala tete ambalo halina budi kujadiliwa kwa kuwa linatugusa katika
maisha yetu ya kila siku.
Nasema
linatugusa kwa kuwa kila binadamu kuna kitu anachoabudu na katika hilo
wapo wapagani ambao hawana dini, wapo wanaoabudu dini za jadi na wapo
wanaoabudu dini mbalimbali lakini katika yote Biblia inasema kitu
chochote ambacho mwanadamu anakiweka mbele kuliko Mungu basi huyo ndiye
Mungu wake hivyo basi kwa mantiki hiyo hakuna ambaye hana Mungu.
Ili kupata ukweli wa tarehe, mwezi, mwaka na siku sahihi ya kuja Bwana
Yesu na mwisho wa dunia hebu tuiulize Biblia inayoaminiwa na wakristo
wengi na wasio wakristo duniani. Biblia inasema katika kitabu cha
Mathayo 24:3 – 6, Hata alipokuwa meketi katika mlima wa Mizeituni
Wanafunzi wake wakamwendea kwa faragha wakisema tuambie mambo hayo
yatakuwa lini, nayo ni nini dalili ya kuja kwako na ya mwisho wa dunia?
Yesu akajibu akawaambia, angalieni mtu asiwadanganye kwa sababu wengi
watakuja kwa jina langu wakisema mimi ni Kristo, nao watawadanganya
wengi, nanyi mtasikia habari za vita na matetesi ya Vita, angalieni
msitishwe, maana hayo hayana budi kutokea, lakini ule mwisho bado.
Hapa
tunaona kwamba habari za mwisho wa dunia hazijaanzia kwetu, kumbe
zilianza toka kwa wanafunzi wa Yesu ambao walitaka kujua ukweli wa Mambo
hayo, wanahoji mambo hayo yatakuwa lini na dalili za kuja kwa Yesu na
mwisho wa dunia? Lakini Yesu anajibu kwamba
waangalie mtu asiwadanganye kwa sababu wengi watakuja wakidai wao ni
akina Kristo na kwamba watawadanganya wengi na pia anawaambia
watayasikia matetesi ya Vita wasitishwe kwani ule mwisho bado.
Pia
Yesu anatahadharisha kuwa tusitishwe kwa kuwa tutasikia Matetesi ya
vita lakini mwisho wa dunia bado. Hapa Yesu anagusia dalili za kuja
kwake na mwisho wa dunia kuwa ni pamoja na matetesi ya Vita na
kuthibitisha kuwa kuna mwisho wa dunia lakini hauji kiuzushi kama watu
wanavyozusha hivyo bado anawaasa watu kutokuwa na hofu na ujio wake.
Ukiendelea
katika mstari wa 7 katika kutaja dalili za ujio wake na mwisho wa dunia
anasema Taifa litaondoka kupigana na Taifa, Ufalme kupigana na Ufalme,
kutakuwa na njaa na kutakuwa na matetemeko ya Nchi na mahali mahali.
Dalili hizi zinazoelezwa na Biblia zimetokea sana na kukaririwa katika
bongo za watu wengi ambapo hadi hivi leo dunia imeshuhudia vita nyingi
sana na ni nchi chache sana duniani ambazo hazijawahi kupigana Vita.
Matetemeko
ya ardhi ndio usiseme na hivi karibuni lilitokea tetemeko la ardhi
Nchini Haiti na kuua watu wengi, upande wa njaa Nchi nyingi duniani
zinakumbwa na njaa na watu wanakufa kwa njaa. Katika mstari wa 11 Yesu
anasema Manabii wengi wa uongo watatokea ns kuwadanganya wengi. Kuhusu
Manabii wa uongo nimekwisha kueleza na nikagusia kuhusu akina Kibwetere.
Pia
katika sura hiyo ya Mathayo 24 anasema kwa sababu ya kuongezeka Maasi
upendo wa wengi utapoa ambapo katika hili tumeshuhudia ndugu wakiuana
kwa sababu ya mali huku wengine wakiwatoa watoto wao kafara kwa kuuwaua
kikatili kwa sababu ya mali .
Ukifuatilia
vyombo vya habari ndugu msomaji kuna mambo mengi ya kutisha
yanayofanywa na wanadamu ambayo hata Shetani mwenyewe yanamshangaza.
Nimewahi kusoma simulizi ya jamaa mmoja aliyeuwa watoto wake wawili,
mama yake na kisha kuzini na maiti ya Msichana mrembo aliyemuua ili
apate utajiri. Ni simulizi ya kutisha ambayo Jamaa huyo alizini na maiti
inayotoa harufu huku sauti ya Jini ikimwambia atakuwa milionea kwa
kutimiza masharti ya kishirikina.
Anasema
wakati huo mtu akiwaambia tazama, kristo yupo hapa, au yuko kule
msisadiki kwa maana watatokea Makristo wa wa uongo na Manabii wa uongo
nao watatoa ishara kubwa na maajabu wapate kuwapoteza yumkini hata walio
wateule. Labda nihoji, hadi naandika Makala hii kuna Yesu wangapi wa
uongo waliokwishaibuka? Bila shaka ni wengi.
Biblia
inaendelea kusema “Tazama nimekwisha kuwaonya mbele, basi wakiwaambia,
yuko jangwani msitoke, yumo nyumbani msisadiki, kwa maana kama vile
umeme utokavyo Mashariki ukaonekana hata Mangharibi hivyo ndivyo kutakavyokuja kwake Mwana wa Adamu.
Hiyo
ni hoja ya msingi sana kwamba Yesu atapokuja ataonekana na watu wote
kama vile Umeme kwani huko mbele tutashuhudia maajabu makubwa zaidi ya
haya tunayoyaona ambapo shetani ataigiza kuja kwa Yesu na kutoa maagizo
yaliyo kinyume na Mungu huku akihalalisha na kubariki uovu.
Yesu atapokuja ataonekana na watu wote lakini Yesu huyu wa bandia ataonekana baadhi ya maeneo. Mathayo 24:36 inasema “Walakini kwa habari ya siku ile na saa ile hakuna ajuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana (Yesu) ila
baba(Mungu) peke yake. Sasa nihoji hao wanaotabiri kwa kutaja tarehe,
mwezi, siku na mwaka wa kuja yesu uhakika huo wanautoa wapi wakati
Biblia inasema hata Yesu mwenyewe hajui.
Lakini
hoja ya msingi Biblia inasema wanadamu wanapaswa kujiandaa na ujio wa
Yesu kwa kuwa hawajui atakuja lini ambapo Mathayo 24: 42 anasema
“kesheni basi kwa maana hamjui ni siku ipi atakayokuja Bwana (Yesu)
wenu. Ifahamike kuwa kukesha kunakoelezwa hapa si kukesha kwa kukaa
macho la hasha bali kuwa tayari kwa kutenda mema muda wote. (Biblia
katika sura ya 24 ya Mathayo)
Kauli
hii ya Yesu inashabiina na usemi maarufu sana usemao ishi katika maisha
ya dunia kana kwamba utaishi miaka 100 ijayo na kidini ishi kama
utakufa leo, kauli hiyo inamaanisha kwa maisha ya kidunia fanya mambo ya
maendeleo kwa matarajio ya kuendelea kuwepo duniani muda mrefu na kwa
maisha ya dunia ujiandae kana kwamba utakufa leo.
Kikubwa
tunachopaswa kutambua ni kwamba dalili nyingi za kuja kwa Yesu na
mwisho wa dunia zimetimia na zinaendelea kutimia na kwamba yuko jirani
kuja na si kwamba ule mwisho umefika bali “U karibu kufika, lakini pia
hawapaswi kuishi kwa hofu kwani Yesu ni mtu wa upendo.
Ifahamike
kuwa dunia haitaangamizwa kwa Vita kama wanasayansi wanavyodai na pia
mwisho wa dunia hautakuja kwa dunia kugongana na Sayari nyingine bali
itaangamizwa kwa moto kwa maana watenda mabaya wataangamizwa kwa moto (
Ufunuo 20: 12 – 15) Ikumbukwe pia dunia ya kwanza wakati wa Nuhu
iliangamizwa kwa maji na baada ya dunia kuangamizwa kutakuwa na Mbingu
mpya na Nchi mpya na Mji mtakatifu Yerusalemu piya utaoshuka kutoka
Mbinguni (Ufunuo 21: 1 – 2)
MWISHO.
Mwandishi wa Makala hii anapatikana kwa simu-0755/0655 761195
Barua pepe-josephmwambije@yahoo.co.uk
TUYALINDE NA KUYATUNZA MAZINGIRA ILI KUIFANYA DUNIA KUWA MAHALI SALAMA PA KUISHI
Na Joseph Mwambije
Songea
Katika vitu muhimu hapa duniani ni suala la mazingira kwa kuwa linagusa maisha yetu ya kila siku na
kwa umuhimu wake basi hata Vitabu vya
dini vimeligusia ambapo Biblia takatifu kwa kugusia inasema baada ya kuwaumba Adamu na Eva Mungu
aliwaweka katika Bustani ya Edeni ili wailinde na kuitunza.
Dunia ilipotoka mikononi mwa Muumba wake ilikuwa ikipendeza
kweli kweli na kumvutia kila mtu kuikaa lakini uharibifu wa mazingira
umetufikisha hapa tulipo ambapo binadamu wamekuwa wakiharibu mazingira bila
hata huruma kwa dunia ambayo wao ni wakaaji ambapo kutokana na hilo Taasisi
mbalimbali pamoja na wanaharakati wa
mazingira wamekuwa wakipigia kelele uharibifu wa mazingira.
Uharibifu wa mazingira umekuwa ukichangiwa na vitendo na
tabia za binadamu katika kukata miti ovyo,kutengeneza mkaa lakini pia kwa Nchi
zilizoendelea uharibifu wa mazingira umekuwa ukichangiwa kwa kiasi kikubwa na
viwanda ambapo moshi wake umekuwa ukiwaathiri binadamu kiafya kwa
kuwasababishia magonjwa mbalimbali ukiwemo ugonjwa wa kansa.
Ukipita vijijini leo misitu ya asili imebaki vipara kutokana
na ufyekaji wa miti ovyo usiozingatia falsafa ya kata mti panda mti unaofanywa
na baadhi ya watu wasio wastaarabu ambao
wanayaharibu mazingira kana kwamba wao watakwenda kuishi kwenye
Sayari nyingine
tofauti na hii wanyoiharibu.
Lakini pia kwa sasa dunia imeendelea sana na baadhi ya Nchi zimekuwa zikitengeneza silaha
nzito ambazo nazo kwa namna moja au nyingine zimekuwa zikiharibu mazingira kwa
kutoa moshi mapiganoni au katika majaribio.
Lakini tukizungumzia katika mazingira yetu katika Mkoa wetu wa Ruvuma na Nchi kwa ujumla kwa
kiasi kikubwa uharibifu wa mazingira umekuwa ukifanyika kwa kuchoma mkaa na
kukata miti ovyo na athari zake zimeshaanza kujionyesha na hili ni dhahiri
kwamba athari za uharibifu wa mazingira zinatishia viumbe hai wakiwemo wanyama na binadamu.
Kutokana na uharibifu huo wa mazingira tumekuwa hatupati mvua za kutosha na hilo lipelekea kukosa mazao ya kutosha na
kutishia kuingiliwa na janga la njaa na
tusipochukua hatua za tahadhari huko mbeleni
Nchi yetu inaweza kugeuka jangwa siku si nyingi.
Nimeanza kwa kuinukuu Biblia kwamba Mungu alipowaumba Adamu
na Eva aliwapa Bustani ya Edeni wailinde na kuitunza si kuiharibu na kama
wangeamua kuharibu mazingira basi sisi wa vizazi hivi vinavyoharibu mazingira
visingeikuta kwa mantiki hiyo basi ni wajibu wa kila mmoja kuyatunza mazingira
ili kuifanya dunia kuwa mahali pazuri pa kuishi.
Sidhani kama kuna mtu akipewa nyumba ili ailinde na kuitunza
na badala yake yeye akaamua kuiharibu hivyo basi tuna kila sababu ya msingi ya
kubadili tabia na kuacha kuharibu mazingira na badala yake tuyalinde na
kuyatunza.
Hapa Songea imezoeleka kuwepo na kampeni za upandaji miti
pasi na mikakati ya kuiendeleza miti iliyopandwa na utamaduni huu ubadilishwe
wa kampeni ya kupanda miti bila kuendeleza huku kampeni za kupanda miti
zikigharimu pesa nyingi bila mafasnikio ya kuiendeleza miti iliyopandwa.
Nafikiri kunapofanyika kampeni za upandaji miti kuwepo na
tahmini ya miti iliyopandwa awali je ni
miti kiasi gani iliyoharibika na mikakati ikoje kuwadhibiti wanaoharibu miti
pamoja na kuwachukulia hatu wafanyakazi wa Taasisi ya misitu wasiwajibika kati
utunzaji wa mazingira.
Suala la mazingira ni pana sana,kwa upande mwingine Halmashauri
ya Manispaa ya Songea inapaswa kuwajibika katika utunzaji
wa mazingira ya viunga vya mji wa Songea kwa kuondoa taka zilizolundikana
katika Manispa hiyo na kusababisha magonjwa ya mlipuko.
Hivyo basi katika kampeni ya mazingira hebu kila mwananchi
aone kwamba kutunza mazingira ni suala
la kila mmoja si la viongozi pekee na
tuache kutupa taka ovyo ili kuzuia magonjwa ya mlipuko.
Hivyo
basi ni wajibu wetu sote kushirikiana kwa kuyalinda na kuyatunza
mazingira ili kuifanya dunia kuwa mahali salama na pazuri kwa kuishi
ambapo patamvutia kila mmoja wetu na si kumchukiza.
Mwisho
Saturday, July 21, 2012
TUJIKUMBUSHE,ZIARA YA PINDA RUVUMA
Waziri Mkuu Mizengo Pinda, akiwa na Viongozi wa Mkoa wa Ruvuma wakati akikagua hifadhi ya chakula ya Taifa,wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Said Mwambungu .Wa pili kulia ni Meneja wa Wakala wa hifadhi ya chakula Bw. Morgan Mwaipyana.
Hapa anafurahia ngoma ya Beta iliyokuwa ikitumbuizwa na Kikundi cha Beta cha Lizaboni Songea.
Akikagua shamba l kahawa toka kwa Mwekezaji huyo wa Kampuni ya AVIV.
Hapa akikagua Shamba la Kahawa la Mwekezaji Bw. Medappa(Katkati) wa Kampuni ya AVIV.wa kwanza kulia ni RC wa Ruvuma Bw. Mwambungu.
Akimwelekeza jambo Mwekezaji.
Akikagua miche ya Kahawa toka kwenye shamba la Mwekezaji.
Hapa anafurahia ngoma ya Beta iliyokuwa ikitumbuizwa na Kikundi cha Beta cha Lizaboni Songea.
Akikagua shamba l kahawa toka kwa Mwekezaji huyo wa Kampuni ya AVIV.
Hapa akikagua Shamba la Kahawa la Mwekezaji Bw. Medappa(Katkati) wa Kampuni ya AVIV.wa kwanza kulia ni RC wa Ruvuma Bw. Mwambungu.
Akimwelekeza jambo Mwekezaji.
Akikagua miche ya Kahawa toka kwenye shamba la Mwekezaji.
MAJENGO MAPYA YAPENDEZESHA TASWIRA YA MJI WA SONGEA
Majengo mapya yanazidi kupendezesha taswira ya Mji wa Songea ,pichani ni jengo la Ofisi za Hazina Mkoa wa Ruvuma.
Jengo la Watawa Wabenediktine wa Hanga ambalo ujenzi wake unaendelea.
Jengo la Watawa Wabenediktine wa Hanga ambalo ujenzi wake unaendelea.
AJALI YA BOTI ZANZIBAR:Gunia liliniokoa
AJALI YA BOTI ZANZIBAR:Gunia liliniokoa |
Mwambinge ambaye amelazwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja, Zanzibar alisema: “Sijui kuogelea, lakini nilikaa kwenye maji kwa saa nne. Nilichoka na kukakata tamaa, nikajiachia ili ikiwezekana nife, lakini nashangaa leo hii ni mzima.” Mtumishi huyo Tume ya Atomiki ambaye alikuwa safarini kuelekea Pemba kikazi, alisema aliokolewa akiwa hajitambui... “Ninachokumbuka ni kwamba waokoaji walinifunga kamba shingoni nikapata maumivu makali, nikapiga kelele wakaniachia, nikatumbukia tena kwenye maji na baadaye walifanikiwa kuniokoa na kuniweka kwenye boti.” Alisema wakati akiwa katika harakati za kujiokoa, aliwaona watu kadhaa wakiwa wamekufa wakiwamo watoto. Kwa upande wake, Ali alisema baada ya meli kuzama na yeye kutupwa nje, aliona gunia na kulidaka. Anasema alilishikilia kwa zaidi ya saa mbili kabla ya kuonwa na vikosi vya uokoaji. Abiria mwingine mkazi wa Bagamoyo, Hamisa Akida alisema meli hiyo ilizama ghafla na haikuwa rahisi kuwa na maandalizi ya kujiokoa: “Kwa jinsi meli hiyo ilivyozama ghafla haikuwa rahisi kujiokoa, kilichotokea hadi tukaokolewa ni mapenzi ya Mungu,” alisema. Alisema hali alipookolewa alikuwa ameshakunywa maji mengi na kuishiwa nguvu... “ lakini nashukuru ni mzima.” Waliopatikana jana Wakati majeruhi hao wakieleza hayo, jitihada za vikosi vya uokoaji hadi jana zilifanikisha kupatikana kwa miili 68 na kati ya hiyo 16 ilitambuliwa. Waliotambuliwa ni Husna Ali Hamis (34) na Kulthum Haji Khamis (34) wote wakazi wa Bagamoyo na Sichana Pandu (45 wa Kilimahewa Zanzibar). Wengine ni Nadra Maulid Mkubwa (17) wa Chumuni, Zanzibar, Mwanaidi Abdallah Ramadhani (21) wa Morogoro, Zubeda Jumanne Kwagaya (26- Meya), Idd Masoud Omari (Miezi 7- Tomondo) Riziki Mohamed Idd (21- Fuoni Zanzibar), Mwanaisha Khamis Haji (75) na Amina Shabani Kibega (24) wote wa Jang’ombe, Zanzibar. Pia wamo Laki Victor Kadoro (28- Mbagala, Dar es Salaam), Damas Leo Mlima (54- Shangani), Halima Sharifu Abdala (21-Kigamboni, Dar es Salaam), Ali Juma Ali (44- Jang’ombe, Zanzibar), Raya Ramadhani Hasani (2- Shakani) Mwanaisha Omari Juma (20- Bunju, Dar es Salaam) na Maryam Idd Omari Omari (25) Shakani. Washindwa kutambua miili Hali katika Viwanja vya Maisara, wanakohifadhiwa maiti jana kulikuwa na mkanganyiko baada ya wananchi wengi kushindwa kuwaona ndugu zao ambao walikuwa wamesafiri katika meli hiyo wakiwamo raia wa kigeni. Maiti moja ya raia wa Kenya imetambuliwa na ndugu zao ambao hata hivyo, walisema wamechanganyikiwa kuhusu namna ya kusafirisha mwili kwenda kwao. Mmoja wa ndugu, John Mumee alisema wameitambua maiti ya ndugu yao aitwaye Martina Masela... “Lakini hatujui tutaisafirisha vipi kwenda Mombasa kwa sababu hatuna fedha, lakini pia hatuelewi tutasafirisha kwa njia gani kwa sababu mashirika ya ndege hayataki kusafirisha maiti.” Alisema marehemu alikuwa akisafiri na mumewe, Bernard Kalii kutoka Dar es Salaam kwenda Zanzibar wakiwa na ndugu mwingine, Mary Kioko ambao bado hawajapatikana. “Tumepata maiti hiyo moja lakini wenzake wawili bado hatujawapata, hatuelewi tufanye nini hapa tumechanganyikiwa tunaomba msaada wa haraka,” alisema Mumee. Waliiomba Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kuwasiliana na Ubalozi wa Kenya nchini ili kuona kama kuna uwezekano wa kuwasaidia kuisafirisha maiti hiyo ambayo alisema imeanza kuharibika. Mkazi wa Temeke, Dar es Salaam, Ali Mzee Moto alisema, hadi sasa hajawaona binti yake, Mwamini Ali aliyekuwa na mtoto wake mchanga. “Walisafiri na meli hiyo na walikuwa wakipitia Zanzibar ili siku inayofuata waende Pemba. Alikuwa anamfuata mchumba wake lakini Mungu hakupenda afike huko,” alisema Moto. Alishangazwa na shughuli ya uokoaji kusuasua na kuhoji sababu za Serikali kushindwa kuomba msaada wa waokoaji kutoka nje. “Tunafahamu ndugu zetu watakuwa wamekufa, lakini tunachoomba sisi ni kupata miili yao ili twende tukawazike,” alisema Moto. Mwingine aliyepotelewa na mtoto ni Philip Cassian John anayefanya kazi Trans Cargo, Dar es Salaam alisema, hajamwona mwanaye Thobias Joseph, anayefanya kazi katika Kampuni ya Hugo Domingo aliyesafiri na meli hiyo kwa safari za kikazi. “Walisafiri na wafanyakazi wenzake ambao maiti zao zimepatikana, sasa niko hapa kusubiri kati ya watakaookolewa leo kama nitamwona mwanangu.” Maiti zaharibika Kati ya maiti 68 zilizoopolewa baharini, 10 hazikutambuliwa na zilizikwa jana na SMZ katika makaburi ya Kama huko Bububu, Zanzibar. Mwenyekiti wa Kamati ya kushughulikia mazishi, Abdallah Twalib alisema maiti zimeharibika vibaya. “Hata baadhi ya ndugu waliozitambua maiti zao wameiomba Serikali izike kwenye makaburi ya eneo la Kama baada ya kuharibika vibaya,” alisema. Sijiuzulu ng’o Juzi, Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu wa Zanzibar, Hamad Masoud Hamad alisema hawezi kujiuzulu kwa tukio hilo kwa kuwa ni mapenzi ya Mungu. Hamad alisema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari akiwa na mawaziri wenzake wanne kutoka katika Serikali ya Muungano na wa SMZ. Hao walikuwa Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, Waziri wa Habari na Michezo wa SMZ, Ali Mbarouk na Waziri wa Katiba na Sheria SMZ, Aboubakar Hamis. Alipoulizwa kama ana mpango wa kujiuzulu kutokana na ajali hiyo ambayo ni ya pili kutokea katika kipindi cha mwaka mmoja, Hamad alisema: “Hivi ningezuiaje upepo usitokee? Ajali hii ni mapenzi ya Mungu kwani haiwezi kuzuiliwa na binadamu kwa sababu imetokana na upepo mkali na ilitokea ghafla, katika kipindi kisichozidi dakika tano meli ilikuwa imezama,” alisema Hamad. “Kujiuzulu siyo utatuzi wa tatizo, bali ni kumwomba Mungu atuepushe na majanga kama haya ambayo hayawezi kuzuiwa na binadamu.” Waziri huyo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa anayetokea Chama cha CUF alisema, kauli za kumtaka ajiuzulu ni mbinu chafu za kisiasa zinazofanywa dhidi yake ili aonekane hafai kuongoza. “Walinipiga vita hata kwenye ajali ya meli ya Mv Spice Islander wakitaka nijiuzulu lakini hata majibu ya tume iliyoundwa kuchunguza ilinisafisha kwamba sihusiki,” alisema. Dk Mwakyembe alisema Watanzania hawana sababu ya kumtafuta mchawi wa ajali hiyo kwani imetokea kwa bahati mbaya... “Tukubali kwamba ajali hii ni bahati mbaya. Maofisa wetu wametuthibitishia bila kuwa na shaka kwamba meli ilikuwa nzima na haikuzidisha abiria, kujiuzulu siyo suluhisho, tushikamane katika kipindi hiki kigumu.” Uzoefu wa mabaharia Mmoja wa mabaharia katika Kivuko cha Bandari ya Dar es Salaam, John Peter amesema Serikali inapaswa kulaumiwa kwa tukio hilo. Peter ambaye amekuwa baharia kwa miaka 24 sasa alisema, pamoja na Serikali kuwa na wataalamu wa kukagua vyombo hivyo kabla, ufisadi katika usajili wa meli bado ni tatizo. “Kama Marine Suveyer (Mtafiti wa Meli) angetekeleza majukumu yake, naamini tusingekuwa na meli mbovu kama hizi,” alisema. Baharia mwingine mwenye uzoefu wa miaka 40, maarufu kama Kepteni Magamba alisema anayepaswa kulaumiwa katika ajali hiyo ni kiongozi wa safari za meli. Kiongozi huyo (Port State Controller) hupokea taarifa kutoka mamlaka ya hali ya hewa na kuruhusu meli iondoke au isiondoke. Kiongozi huyo husimamia usalama wa meli ndani na nje ya bahari kwa kushirikiana na eneo meli inapoelekea. “Meli kabla ya kuondoka lazima ifuate taratibu zote, nahodha hupata kibali kutoka Sumatra (clearance) na kuipeleka kwa ‘Port State Controller’ ambaye tayari anakuwa ameshapata taarifa za hali ya hewa,” alisema Magamba. Wanasiasa Vyama kadhaa vya siasa vimetoa salamu za pole kwa wafiwa na kuishauri Serikali kuongeza umakini katika ukaguzi wa vyombo vya baharini. Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba aliitaka Serikali kuangalia upya uwajibikaji, utendaji na mwenendo wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) akidai kuwa taasisi hiyo imeshindwa kuwajibika ipasavyo kudhibiti vyombo vya usafiri. Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbrod Slaa ameshauri kanuni za Bunge zinazotumika hivi sasa kuangaliwa upya ili kuruhusu Bunge kujadili ajali hiyo... “Nimesikitishwa na kitendo cha Naibu Spika (Job Ndugai) kuzuia wabunge kujadili suala la kuzama kwa meli bungeni kwa maelezo kuwa kanuni haziruhusu. Nitoe wito kwa kanuni kuangaliwa upya ili kuruhusu Bunge kujadili masuala ya kitaifa pindi yanapotokea.” Mwenyekiti wa APPT Maendeleo, Peter Mziray alisema: “Lipo tatizo katika uingizaji, ukaguzi na usajili wa vyombo vya usafirishaji wa majini… Serikali na mamlaka zinazohusika na usajili hazifanyi kazi kwa kuzingatia umuhimu wa kazi waliyopewa na matokeo yake ndiyo kuruhusu vyombo vibovu kubeba roho za watu.” Sumatra yajitetea Hata hivyo, Sumatra imejitetea kwamba haitambui usajili wa boti hiyo ya Mv Skagit. Meneja Uhusiano wa Sumatra, David Mziray alisema meli hiyo ilisajiliwa na Mamlaka ya Usafiri wa Majini Zanzibar (ZMA). Alisema meli hiyo ilipewa cheti cha ubora na mamlaka hiyo Agosti, 24 mwaka jana ambacho kinamalizika muda wake, Agosti 23, mwaka huu ikiwa na uwezo wa kubeba abiria 300 na tani 26 za mizigo... “Hatuwezi kutoa maelezo zaidi kwa sababu ilisajiliwa Zanzibar na si huku kwetu.” Habari hii imeandikwa na Burhani Yakub, Pangani; Raymond Kaminyoge na Salma Said, Zanzibar; Kelvin Matandiko, Nora Damian, Joyce Mmasi, Geofrey Nyang’oro na Aidan Mhando Dar. |
Friday, July 20, 2012
MENEJA WA MELI ILIYOZAMA ZANZIBAR AKAMATWA
Meneja meli iliyozama Zanzibar akamatwa |
FIKIWA WATU 63, SERIKALI YATANGAZA SIKU TATU MAOMBOLEZO | ||
JESHI
la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia Omari Hassan
Mnkhon ambaye ni Meneja wa boti ya Mv Skagit, kwa ajili ya mahojiano
baada ya kubainika kwamba kumekuwa na kasoro za kumbukumbu katika
taarifa za hiyo.Wakati Jeshi hilo likimshikilia meneja huyo, hadi jana
jioni saa 10:30, vikosi vya uokoaji vilifanikiwa kupata maiti 63, huku
29 kati yao ikiwa imetambuliwa majina namba za tiketi na sehemu
wanakotoka marehemu. Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa meneja wa boti Mkoa wa Dar es Salaam, anashikiliwa ili kuweza kusaidia jeshi la polisi kupata taarifa za kina kuhusu za meli hiyo. Kova alisema tukio hilo linagusa maeneo mengi ikiwa ni pamoja na Mkoa wa Dar es Salaam ambako safari za meli hiyo huanzia na kuongeza kwamba, wanamshikilia meneje huyo baada ya kukosekana taarifa muhimu juu ya safari za boti hiyo. “Tunamshikilia meneja wa meneja hiyo ili atusaidie kutupa taarifa za kina, kwani tukio hilo sio dogo na uchunguzi wa kina unatakiwa kufanywa,” alisema Kova na kuongeza; “Jeshi la polisi litafanya uchunguzi wa kina kwa kushirikiana na vyombo na mamlaka zinazohusika, ili kujua chanzo cha ajali pamoja na kupata taarifa za kina za boti hiyo tangu ilipoanza safari yake,” alisema. Maiti zilizotambuliwa Hadi saa 10 jioni jana, maiti 63 zilikuwa zimepatikana na watu 145 kuokolewa wakiwa hai. Hata hivyo kati ya maiti hizo zilizopatikana, matiti 34 zilichukuliwa na ndugu zao. Baadhi ya maiti waliotambuliwa pamoja na umri wao na maeneo wanayoishi katika mabano ni Anita Emanuel (42, Kibamba -Dar es Salaam), Rukiya Issa Muombwa (miezi 2, Meli nne –Fuoni Zanzibar ), Halima Ali Khamis (23, Mtopepo- Zanzibar), Kolin Krispin (miezi 9, Kunduchi - Dares Salaam) na Rahma Ali Abdalla (miaka 52, Mfenesini - Zanzibar). Maiti wengine ni Said Jumanne Masanja (miaka 9, Nzega Tabora), Sauda Abdalla Omar (22, Ole Pemba), Said Juma Said (36, Arusha), Amina Abdalla Tindwa, (miezi 6, Fuoni), Halima Ramadhani Kilimo, (53, Morogoro), Khadija Omar Ali (58), Amina Hamir Bakari (39, Chukwani - Zanzibar), Mwanahamisi Mshauri (42, Kibandamaiti), Ali Hamdu Othman (35, Mkwajuni) na Mohamed Said Salum (40, Magomeni Mikumi - Dares Salaam). Wengine ni Amina Ahmed Ramadhani (21, Michenzani zanzibar ), Mgeni Juma Halfani (25, Daraja Bovu), Khadija Rajab Kibune (22, Fuoni), Maua Ramadhani Feruzi (29, Mwembeladu), Hussein Ali Khamis (4, Mwanakwerekwe) na Sabiha Heri Mbarouk (25, Mgeleme, Chakechake-Pemba). Pia wamo Halima Ali Mohamed (35, Kiwengwa- Zanzibar), Asia Juma Khamis (29, Kiembe Samaki), Yusuf Hasan Yusuf (7, Chamanzi, Dar es Salaam), Batuli Abrahmani Amir (20, Jang'ombe), Fatma Said Sultani (54, Msasani Dar es Salaam), Juma Jafari Shajak (Miezi 6, Kimaneta - Tanga) na Mohamed Ali Ngombe (41, Buguruni - Dares Salaam). Serikali yatangaza siku tatu za maombolezo Kufuatia msiba huo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imetangaza siku tatu za maombolezo kuanzia Julai 19 hadi Julai 21 mwaka huu. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohammed Shein alisema bendera zote zitapepea nusu mlingoti na shughuli zote zinazoambatana na sherehe na burudani zimefutwa kwa muda huo lakini kazi na shughuli za Serikali zitaendelea kama kawaida Nayo Serikali kupitia kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi ilitangaza siku tatu za maombolezo kufuatia msiba huo mkubwa uliolikumba taifa. Lukuvi aliwaambia waandishi katika kipindi hicho cha siku tatu bendera zitapepea nusu mlingoti na shughuli za starehe zitasimamishwa ila kazi zitaendelea kama kawaida. Rais Shein amewahakikishia wananchi na hasa waliopoteza jamaa zao kuwa Serikali itabeba gharama zote za mazishi na huduma za matibabu kwa majeruhi. “Nimesikitishwa sana na msiba huu. Katika wakati huu si vema tukaanza kulaumiana jambo la muhimu hivi sasa ni kuokoa maisha ya watu,” alisema Rais Dk Shein. Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick alisema kutokana na maagizo ya Waziri Mkuu aliyoyatoa Bungeni Mkoa wa Dar es Salaam ndio umepewa jukumu la kushuhulikia suala hilo. Alisema kwa sasa mkoa Umepanga kutoa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya kuhifadhi mili ya watu waliofariki katika ajali hiyo. “Tumepanga kwamba, Hospitali ya Taifa Muhimbili ndio itahusika katika kuhifadhi miili ya watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo,” alisema Sadick na kuongeza; “Watu wote ambao wanajua kuwa ndugu zao walisafiri na meli hiyo wafike katika bandari ya Dar es Salaam kwa ajili ya utambuzi,” alisema na kuongeza kuwa ambayo haitatambuliwa Serikali itachukua jukumu la kuizika. EU yatoa ndege ya uokoaji Katika kuonyesha kuguswa na ajali hiyo, Umoja wa Ulaya (EU) umetoa ndege maalum kusaidia juhudi za utafutaji na uokoaji katika eneo la ajali. Balozi wa Uingereza hapa nchini Diane Corner aliwaambia waandishi wa habari mjini Zanzibar kuwa wameamua kutoa msaada wa ndege hiyo ambayo iliwasaili Zanzibar usiku wa kuamkia Julai 19, kitokea katika visiwa vya Ushelisheli. “Hii ni ndege maalum ambayo kazi yake ni kuratibu na kubainisha eneo ambalo kuna watu na inawasiliana na waokoaji walioko majini ikiwa angani,” alisema Balozi Corner. Alifafanua kwamba, Umoja wa Ulaya unaendelea kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) katika kazi ya uokoaji, lakini pia Umoja huo upo tayari kutoa msaada wowote utaohitajika. Kwa upande wake, Balozi wa Marekani nchini, Leahant Alfonso alisema Serikali yake imetoa msaada wa dawa kwa ajili ya watu waliojeruhiwa katika ajali hiyo. Balozi Alfonso aliipongeza SMZ kwa kuchukua hatua haraka kukabiliana na maafa hayo. “Nawapa pole watu wa Zanzibar kwa msiba huu, nimesikitishwa na kuhuzunishwa sana, hasa nilipoziona maiti saba za watoto wadogo. Moyo wangu umeumia sana,” alisema huku akibubujikwa machozi. Wabunge wachangia maafa Katika hatua nyingine, wabunge wote watakatwa posho ya siku moja kuchangia maafa ya kuzama kwa boti hiyo huku Bunge likiahirishwa kwa siku moja kuomboleza maafa hayo. Posho hizo za wabunge zitawezesha kupatikana kwa Sh24.6 milioni kutoka kwa Wabunge wa sasa 352 ambao kila mmoja atachagia Sh70,000. Spika Anne Makinda jana asubuhi aliahirisha shughuli za Bunge kwa siku moja na kutangaza kuwa, Kamati ya Uongozi ya Bunge katika kikao chake jana asubuhi, iliamua zikatwe posho za siku moja na fedha hizo zitatolewa kama rambirambi kwa ndugu wa watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo. Wakizungumza baada ya ajali hiyo, baadhi ya wabunge waliitupia lawama Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), kwa kile walichodai kuwa ilishindwa kutoa taarifa ya tahadhari kwa watumiaji wa usafiri wa majini. Mbunge wa Mtera (CCM), Livingstone Lusinde alisema mamlaka hiyo inabeba lawama kwa kushindwa kutoa ushauri kwa vyombo husika na badala yake wanafanya kazi ya kutabiri mvua tu. “Wale jamaa hawafai kabisa, matatizo yote wanatakiwa kubebeshwa wao kwa kuwa hawakuweza kutoa ushauri juu ya nini kingetokea mbele ya safari,’’ alisema Lusinde. Mbali na Mamlaka ya Hali ya hewa, lakini mbunge huyo alitaka pia wakaguzi wa vyombo vya majini kuwajibika kwa kushindwa kukagua uimara wa vyombo hivyo. Kwa upande wake Mbuge wa Viti Maalumu (CCM), Martha Mlata alisema tukio la kuzama kwa meli hiyo alilipokea kwa masikitiko lakini akasema “ni kazi ya Mungu.’’ Mlata alisema tangu juzi yeye pamoja na wabunge wengine wako katika maombi mazito ya kutaka Mungu awanusuru majeruhi na kuwapa nguvu ya ujasiri waokoaji ili wafanya kazi yao kwa moyo wa kujituma zaidi. “Unajua tunafanya mambo tangu tulipopata taarifa za ajali hiyo na hadi sasa tunatakiwa kuendelea kufanya maombi hayo kwa ajili yha ndugu zetu, naamini mkono wa Mungu hautapungukia kitu,’’alisema Mlata. Ushuhuda wa mabaharia, waokoaji Akizungumzia ajali hiyo, mmoja wa waokoajii binafsi, waliofika katika tukio hilo alisema boti hiyo imebinuka ikiwa mgongo juu. Mmoja wa wahanga aliyenusurika katika ajali hiyo, Hassan Khatib alisema tangu waliondoka Dar es Salaam mnamo saa 6:00 mchana juzi, hali ya bahari ilikuwa mbaya kwa sababu kulikuwa na mawimbi makubwa baadaye meli ilizidiwa na kupoteza mwelekeo. Alisema baada ya hapo ililala upande na kisha ilibinuka na yeye kutupwa kwenye maji na akawa hana kitu cha kushika ndipo alianza kuogelea na kufanikiwa kushi ubao na kuogelea nao. Alisema huduma uokoaji zilichelewa kufika ila mara baada ya ajali ilifika ndege na kuzunguka katika eneo la tukio na kuondoka na baada ya saa kadhaa vilifika vyombo ukoaji. TMA watoa kauli Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Dk Hamza Kabelwa alisema kuwa, kupitia ofisi yao iliyopo bandarini Dar es Salaam walitoa taarifa kwenye vyombo vya usafiri wa majini juu ya upepo mkali uliokuwa ukivuma baharini kwa kasi ya kilometa tatu kwa saa kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 5:00 asubuhi. “Tulipogundua hali hiyo tulitoa taarifa kwa wahusika wa vyombo vya usafiri wa majini tu,” alifafanua Dk Kabelwa. Meli ya Skagit ilitengenezwa mwaka 1989 nchini Marekani na ilikuja nchini 2008. Shahihisho Jana gazeti hili lilichapisha kwa makosa kuwa meli iliyozama inaitwa MvSkad badala ya Skagit. Habari hii imeandikwa na Boniface Meena, Habiel Chidawali, Dodoma, Salma Said, Zanzibar Aidan Mhando, Pamela Chilongola na Victoria Mhagama, Dar |
KUTANA NA BINGWA WA KUCHEKA TANZANIA
Hapa anatafakri jambo ni namna gani atapata Mtu wa kushindana nae,maana wengi wanamkimbia hata Masudi Sura mbaya alimkimbia kwenye shindano la kumtafuta mwenye sura mbaya Tanzania.
Huyu ni Msanii Bingwa wa kucheka Tanzani na duniani kwa ujumla ambapo ana uwezo wa kucheka kwa dakika 18 bila kupumzika hapa alikuwa akipafomu kabla Waziri Mkuu Mizengo Pinda hajapand jukwaani kuhutubia Wananchi Mkoani ruvuma hivi Karibuni.
Huyu ni Msanii Bingwa wa kucheka Tanzani na duniani kwa ujumla ambapo ana uwezo wa kucheka kwa dakika 18 bila kupumzika hapa alikuwa akipafomu kabla Waziri Mkuu Mizengo Pinda hajapand jukwaani kuhutubia Wananchi Mkoani ruvuma hivi Karibuni.
WAWILI WASHIKILIWA NA POLISI KWA TUHUMA ZA KUMUUA KIKATILI MTOTO WAO MCHANGA KWA KUMNYONGA
WAWILI WASHIKILIWA
NA POLISI KWA TUHUMA ZA KUMUUA KIKATILI MTOTO WAO MCHANGA KWA KUMNYONGA
Na Joseph Mwambije,
Songea
WATU wawili mtu na mkewe katika Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma
wanashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kumuua kinyama kwa kumpiga kwa mawe mtoto
wao mchanga wa Miezi saba na kumuweka kwenye Chemba ya Mtaro wa maji kwa kile kinachodaiwa kuwa ni Masuala ya kimapenzi.
Ofisa Mtendaji wa Mtaa wa Chemchem katika Kata ya Matogoro Mkoani humo Bw. Fama
Suta amewataja wanaoshikiliwa kuwa ni Bw.
Shangwe Komba(28) na Mkewe
Bi. Mwazani Chimgege(25) wakazi wa
Chemchem Matogoro Mkoani humo.
Amewaambia Waandishi wa habari kuwa tukio hilo
lilitokea Julai 16 mwaka huu katika Mtaa
wake ambapo anasema yeye baada ya kufahamishwa kuhusiana na tukio hilo alitoa taarifa Kituo
cha Polisi cha Mjini kati kwa njia ya simu.
Kiongozi huyo wa Mtaa
akisimulia jinsi tukio lilivyosikitisha alisema kuwa kwa jinsi tukio
lenyewe alivyoliona awali mtoto huyo wa kiume alinyweshwa sumu na kunyongwa na kisha kupigwa mawe akiwa
kwenye Mtaro wa Chemba ya kupitishia maji. .
‘Mtoto huyo aliuawa
baada ya kupita wiki moja ya
kufanyiwa tohara na kwa kweli ni tukio linalosikitisha ambapo mimi linanifanya
niweweseke usiku na katika Mtaa wangu hili ni tukio la kwanza’alisema na
kuongeza
Anasema awali Polisi walimkamata Zawadi Komba dada wa
Mtuhumiwa Shangwe Komba na kumuhoji kuhusiana na tukio hilo ambapo alieleza kuwa mdogo wake huyo alimuomba ampe sh. 50,000
akamtibu mwanae huyo wa kufikia aliyemuua.
Alisema baada ya kumpa pesa hiyo akaja na kuomba pesa
nyingine ambapo akasema hana ampeleke kwa pesa hiyo na endapo atalazwa atakuja
Hospitali na baada ya kuelezwa hivyo ndipo akamwambia kuwa amemuua Mwanae
anaomba ampe pes nyingine ili akimbie.
Hata hivyo baada ya kumuhoji Mwanamke huyo na kufanikiwa
kuwakamata Watuhumiwa kwa ushirikiano wake Polisi walimuachia huru.
‘Kwa kweli inaonyesha kuwa Mwanaume huyo alishauriana na Mkewe wamuue mtoto huyo ili waweze
kufurahia maisha yao
na kutafuta mtoto mwingine kwa kuwa mtoto yule hakuwa wa Mwanaume huyo’alisema.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Deudediti Nsemeki
amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kubainisha kuwa uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea ili
kubaini chanzo chake na kuwafikisha Mahakamani Watumiwa.
Tuesday, July 17, 2012
MHANDO WA TANESCO AICHANGANYA SERIKALI NA WABUNGE
Mwishoni mwa wiki, bodi hiyo iliwasimamisha kazi Mhando, Naibu Mkurugenzi Mtendaji, Huduma za Tanesco, Robert Shemhilu, Ofisa Mkuu wa Fedha, Lusekelo Kassanga na Meneja Mwandamizi, Ununuzi, Harun Mattambo. Hata hivyo, baadhi ya wabunge walio katika Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) na wengine wa Kamati ya Nishati na Madini, wamesema uamuzi huo umejaa maswali kuliko majibu. Moja ya maswali hayo ni mchakato wa kumsimamisha wakihoji kikao kilichochukua uamuzi huo kuitishwa na wizara badala ya bodi, kupatikana Mkaguzi Kampuni ya Ernst&Young kukagua hesabu za Tanesco bila kupitia Sheria ya Ununuzi wa Umma na tuhuma za ukabila dhidi ya bosi huyo wa Tanesco. Lakini, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi alipoulizwa jana kuhusu tuhuma hizo za wizara kuingilia mamlaka ya bodi, alijibu: “Kesho (leo) tunakutana na kamati, kwa hiyo siwezi kuzungumza chochote nitazungumza ndani ya kamati.” Hata hivyo, habari kutoka kamati hizo za Bunge zinasema mkutano kati ya watendaji wa wizara, bodi na wajumbe wa kamati hizo unatarajiwa kuwa na mvutano mkali. Tayari baadhi ya wajumbe wa POAC wamehoji tuhuma za ukabila ambazo anatuhumiwa kuwa nazo Mhando, huku wakimnyooshea kidole Maswi na waziri wake. “Hivi Mhando ukabila wake ni nini...? Hivi, tunapaswa kujadili uwezo wa mtu au kabila lake?” alihoji mmoja wa wajumbe wa POAC. Mwenyekiti wa POAC, Zitto Kabwe alipoulizwa kuhusu kikao chao cha kesho alisema tayari wameshamwandikia barua Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na wanatarajia kukutana na bodi kupata ufafanuzi. Kusimamishwa Mhando Hatua hiyo ya kumsimamisha Mhando ilitangazwa mwishoni mwa wiki na bodi hiyo baada ya kikao cha dharura ambacho kilijadili tuhuma mbalimbali dhidi ya menejimenti ya Tanesco. Kikao hicho kiliongozwa na Mwenyekiti wake, Jenerali Mstaafu Robert Mboma na kuchukua uamuzi wa kumsimamisha kazi Mhando ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka. “Hivyo, Bodi iliazimia pamoja na mambo mengine, kama ifuatavyo: Uchunguzi wa tuhuma hizo uanze mara moja kwa kutumia uchunguzi huru na kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Mhandisi William Mhando ili kupisha uchunguzi huo na kwa kuzingatia matakwa ya sheria za kazi nchini,” ilieleza sehemu ya taarifa aliyoitoa Mboma kwa vyombo vya habari. Mhando aliteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco Juni Mosi, 2010 akichukua nafasi ya mtangulizi wake, Dk Idris Rashidi ambaye alimaliza muda wake wa uongozi. Mara baada ya uteuzi huo, Mhando alisema kwamba moja ya mambo ambayo atahakikisha anayatekeleza ni kuhakikisha kuwa wateja wote wa shirika hilo wanakuwa na mita za Luku. Kabla ya uteuzi huo, Mhando alikuwa ni Meneja Mkuu Usambazaji Umeme na Masoko katika shirika hilo. |
FHATUA
ya Bodi ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kumsimamisha kazi
Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, William Mhando imeibua mvutano kati ya
wabunge na Serikali.
WABUNGE VIJANA KUPITIA KJT,NI K KUANZIA MWAKA HUU WA FEDHA
WATATU RUVUMA WANUSURIKA AJALINI BAADA YA GARI KUTUMBUKIA MTONI
Wananchi wakishaa gari iliyoacha njia na kutumbukia katika mto Matarawe.Ktk ajali hiyo watu watatu walijeruhiwa na hakuna aliyepoteza maisha.
Gari hiyo ya mizigo ilikuwa imebeba mahindi na kufuatia ajali hiyo wananchi wameomba daraja la Matarawe lipanuliwe ili kuwanusuru na ajali za mara kwa mara zinazotokea katika daraja hilo
Gari hilo liligonga kingo za daraja na kuingia nazo mtoni.
Wananchi bado hawaamini kilichotokea kwamba abiria wamenusurika kutokana na ajali yenyewe ilivyokuwa
Hapa wakiwa wamekaribia kabisa gari wakishangaa.
Gari hiyo ya mizigo ilikuwa imebeba mahindi na kufuatia ajali hiyo wananchi wameomba daraja la Matarawe lipanuliwe ili kuwanusuru na ajali za mara kwa mara zinazotokea katika daraja hilo
Gari hilo liligonga kingo za daraja na kuingia nazo mtoni.
Wananchi bado hawaamini kilichotokea kwamba abiria wamenusurika kutokana na ajali yenyewe ilivyokuwa
Hapa wakiwa wamekaribia kabisa gari wakishangaa.
Subscribe to:
Posts (Atom)