Saturday, September 22, 2012

Julius Malema matatani kwa utata wake

 Na Mashirika ya habari
Afrika kusini

Julius Maleme
Polisi wa Afrika Kusini wametoa waranti ya kukamatwa mwanasiasa wa Afrika kusini anayeleta utatanishi, Julius Malema, ambaye alifukuzwa kutoka chama tawala cha ANC.
Anatarajiwa kufikishwa mahakamani juma lijalo kuhusu mashtaka ya ku-ghu-shi fedha, rushwa, na wizi kwa njia za udanganyifu.
Kamati maalumu ya uchunguzi, iitwayo "the Hawks", imekuwa ikichunguza shughuli za kibiashara za Bwana Malema.
Bwana Malema, ambaye aliwahi kuwa mfuasi mkubwa wa Rais Jacob Zuma, amegombana na washirika wake wa zamani, na akafukuzwa chamani, kwa kutoa wito kuwa serikali ya Botswana inafaa kupinduliwa.

Friday, September 21, 2012

PIKIPIKI HIZI KWA AJILI YA KUBEBEA WAJAWAZITO BADO ZINAPIGWA NA VUMBI KATIKA HOSPITALI YA MKOA WA RUVUMA

 Hizi ni pikipiki maalumu kwa ajili ya kubebea wajawazito toka maeneo ya vijijini na kuwafikisha hospitalini.



DC SONGEA ATEMBELEA WAFANYABIASHARA WA MITUMBA MAJENGO

 Mkuu wa Wilaya ya Songea Bw. Joseph Mkirikiti akizungumza na mmoja wa Wafanyabiashara wa mitumba  katika Vibanda vya majengo ambako wafanyabiashara hao wamehamishiwa.
Hapa akikagua moja ya vibanda hivyo.Wafanyabiashara wanaofanya biashara za mitumba katikati ya Mji wa Songea wamehamishiwa Majengo.

Tuesday, September 18, 2012

Ugumba wawatesa Watanzania wengi


 

Wauguzi nchini Kenya wakiwa wamewabeba watoto walipatikana kwa njia ya mwananmke kupandikizwa mbegu za kiume, ripoti za nchini kenya zinaonyesha watanzania 60 wamekwenda nchini humo kupata huduma hiyo. Picha na Arthur okwemba
WASAKA WATOTO KENYA KWA SH5.4 MIL, HADI SASA WANAWAKE 60 WAMEHUDUMIWA DAKTARI WA MUHUMBILI AKIRI TATIZO NI KUBWA
Na Mwandishi Wetu,
TATIZO la uzazi linaonekana kushika kasi nchini baada ya idadi kubwa ya wanandoa kukimbilia Kenya kupata huduma ya upandikizaji wa watoto kwa gharama ya zaidi ya Sh5 milioni.Kati ya wageni 10 wanaokwenda katika vituo vya upandikizaji vya Aga Khan na Nairobi IVF Centre nchini humo, wanne wanatoka Tanzania.Licha ya kuwapo kwa huduma hiyo nchini, imeelezwa kwamba Watanzania wengi wanakimbilia huko kutokana na unafuu wa gharama na ubora wa huduma.
Huduma hiyo ni ya mwanamke kupandikizwa mbegu ya kiume ili kuweza kushika mimba na baadaye kupata mtoto.
Mmiliki wa Kituo cha Upandikizaji cha Nairobi (Nairobi IVF Centre), Dk Joshua Noreh alisema kwa mwaka kliniki yake hupokea zaidi ya wagonjwa 270 kutoka mataifa mbalimbali  likiwamo Bara la Ulaya.
Alisema wagonjwa kutoka Tanzania walianza kumiminika katika kliniki hiyo kuanzia mwaka 2006 na ukiondoa gharama za matibabu ambazo ni Sh5.4 milioni zipo gharama za ushauri na uchunguzi wa tatizo.
“Gharama ya ushauri peke yake ni Sh42,000 za Tanzania. Baada ya ushauri, mgonjwa hutozwa Sh420,000 kwa ajili ya uchunguzi wa tatizo. Gharama za matibabu hutegemea ukubwa wa tatizo. Tiba yenyewe ni upandikizaji wa mbegu, hadi hatua za kuirutubisha,” alisema.
Dk Noreh alisema ukijumlisha gharama za usafiri, malazi, mlo na tiba kwa wagonjwa wanaotoka Tanzania, wengi wao hutumia kati ya Sh8milioni hadi Sh10 milioni, kwa ajili ya kupata mimba.
Imeelezwa kuwa raia wa Uganda hukimbilia Kenya kukwepa gharama kubwa kwani nchini humo hugharimu kiasi cha Sh500,000 ya Uganda (sawa na Sh9.5 milioni) wakati huduma hiyo hupatikana Kenya kwa Sh300,000 (sawa na Sh5.4 milioni) kwa mzunguko.
“Tuna vituo zaidi ya vitano vya IVF hapa Kenya, ndiyo maana Kenya imekuwa kimbilio la wanandoa au wapenzi kupata matibabu ya aina mbalimbali za ugumba. Lakini  kikubwa ni huduma bora na gharama nafuu ndiyo sababu ya ongezeko hili la wageni kutoka nje.”
Alisema baadhi ya nchi hazina huduma ya IVF hivyo wanandoa huenda Kenya na wengine wanayo huduma hiyo katika nchi zao ila wanachagua Kenya kwa sababu ya urahisi wa tiba hiyo na kuwapo kwa mbegu za wanaume wa Kiafrika zilizohifadhiwa.
Nchi nyingine ambazo wanandoa wake wanaongoza   kwenda Kenya kwa ajili ya kupata huduma ya upandikizaji wa watoto ni Uganda, Sudan ya Kusini, Marekani na Ethiopia.
Mtaalamu kutoka Hospitali ya Chuo Kikuu cha Aga Khan Nairobi, Dk Prafull Patel alisema idadi ya wanaohitaji huduma hiyo imekuwa ikiongezeka kwa kasi kutoka mataifa ya Afrika, Uingereza na Marekani.
Alisema zaidi ya robo tatu ya wanaopata huduma hiyo ni watu kutoka nje ya Kenya, lakini hasa ni kutokana na unafuu wa gharama za huduma hiyo ikilinganishwa na nchi nyingine.
Nchini Uganda, IVF inagharimu Sh9,000,000 za Tanzania wakati Uingereza inagharimu zaidi ya Sh10,800,000 za Tanzania na kwa wenza zinafikia Sh21,600,000 kwa kila mzunguko huku Marekani ikigharimu Sh10,620,000 na Sh19,800,000 kwa mzunguko.
Hii inamaanisha kwamba gharama nchini Kenya ni nusu ya gharama inayolipiwa Marekani, Ulaya na nchi nyingine za Afrika. Hiyo inaelezwa kuwa chanzo cha ongezeko la idadi ya wageni kwenda Kenya kusaka tiba ya ugumba.

Upandikizaji unavyokuwa
Upandikizaji huo hufanyika kwa kuchukua mbegu za mwanamume na kuzipandikiza katika mirija ya uzazi ya mwanamke.
Mwanamke mwenye matatizo huweza kwenda peke yake kupandikizwa kwa kununua mbegu zilizohifadhiwa katika kliniki au wanandoa kwenda pamoja na mwanamume kutoa mbegu ambazo zitapandikizwa kwa mwanamke.
“Tiba huchukua mwezi mmoja, huanzia siku ya pili baada ya mwanamke kumaliza hedhi na siku ya yai kurutubishwa lakini mwanamume hutumia siku moja tu pale mbegu zake zinapohitajika.”
Dk Noreh alisema sababu ya kuanza tiba siku ya pili baada ya mwanamke kumaliza mzunguko wake wa mwezi ni kulenga tarehe za uchavushaji, kwani kipindi hicho mbegu za mwanamume hupandikizwa na kusababisha mimba kutungwa.
“Mbegu zilizorutubishwa huachwa kwa siku mbili mpaka tano ndani ya chombo maalumu ili kukuza kiinitete (embryo) kabla ya kuhamishwa katika nyumba ya uzazi ya mwanamke kwa ajili ya kutungisha mimba ya kawaida.”
Alisema tatizo la ugumba linaongezeka duniani na njia hiyo inatumika kuwasaidia wanawake wasiokuwa na mayai ambao mirija yao ya kuyasafirishia imeziba na wanaume ambao manii yao ni dhaifu na hushindwa kuogelea hadi kufikia yai la mwanamke...
“Tatizo la ugumba kwa sasa ni wastani wa asilimia 10, hiyo ina maana kwamba kati ya wanandoa 10 mmojawapo hana uwezo wa kushika mimba. Kiwango hiki kwa sasa kinakua kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo wanawake wa sasa kuchelewa kuolewa wakitoa kipaumbele kumalizia masomo,” alisema Dk Noreh.

Wataalamu wa Tanzania
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba cha Muhimbili, Dk Henry Mwakyoma alisema ongezeko la Watanzania kufuata huduma hiyo Kenya, limesababishwa na kukua kwa tatizo la uzazi nchini.
Dk Mwakyoma alisema huduma hiyo hutolewa kama tatizo la uzazi analo mwanamke. Alisema kama mwanamume ndiye mwenye tatizo, huduma hiyo haiwezi kutolewa.
“Kama mwanamke ana tatizo la uzazi, kwa mfano mirija imeziba, kizazi kimelegea, anaweza kufanyiwa upandikizaji na kupata mtoto, lakini kama mbegu za mwanamume ni dhaifu, hakuna kitu kinafanyika,” alisema.
Dk Mwakyoma ambaye aliwahi kufanya utafiti na kubaini kuwa asilimia 80 ya wanaume nchini wana tatizo la ugumba wa kudumu au wa muda, alisema mfumo wa maisha wa sasa ndicho chanzo cha ongezeko la tatizo la uzazi.
Daktari kutoka kituo kimoja cha upandikizaji nchini ambaye hakutaka kutajwa jina, alisema huduma hiyo inapatikana katika kituo hicho kwa bei nafuu kuliko huko Kenya.
“Gharama za hapa zinategemea ukubwa wa tatizo la mhusika, mchakato wake na afya yake. Wapo wengine hawahitaji kupandikizwa, wengine wanahitaji tu dawa, pia wapo wengine wanaweza kufanyiwa upandikizaji kwa zaidi ya mara moja,” alisema.
Alisema tangu kufunguliwa kwa kituo hicho Februari mwaka huu, idadi ya wanandoa wanaokwenda kupata huduma hiyo imekuwa ikiongezeka. Hata hivyo, hakutaka kuweka wazi takwimu rasmi kwa mwezi au tangu kufunguliwa kwake.
CHANZO-GAZETI LA MWANANCHI

Al-Shabaab waanza kutoroka Kismayo

 Na Mashirika ya habari
Somalia
Wanajeshi wa Kenya Kismayo
Wenyeji mjini Kismayo Somalia, wameambia BBC kuwa wapiganaji wa Al-Shabab wameanza kuondoka
katika ngome yao ya mwisho ya Kismayo.
Kismayo ndio ngome kubwa na ya mwsisho ya kundi hilo linalopigana na jeshi la Somalia ambalo limekuwa likiuzingira mji huo kwa usaidizi wa wanajeshi wa AU.
Wenyeji wa mji huo wanasema kuwa wapiganaji wamekuwa wakiutoroka mji huo kwa mabasi huku wakibeba silaha nzito nzito.
Lakini Al-Shabab wamekana ripoti hizo wakisema kuwa wameweza kuwashinda nguvu wanajeshi wa AU.

'Vita vya Propaganda'
Msemaji wa kundi hilo, Muhammad Usman Arus, ameambia BBC kuwa Al Shabaab wamewaua wanajeshi 100 wa Kenya na wa Somalia na kuwaondoa kutoka Kismayo.
"tunadhibiti Kismayo, hizi ni propaganda tu. Wanajeshi wa Somalia na Kenya tayari wameondoka katika maeneo yao'' alisema msemaji huyo.

Wenyeji wa mji huo walisema kuna utulivu ingawa baadhi walidai kuwa kundi hilo limewaacha nyuma vijana ambao wameamrishwa kumuua yeyote anayepinga kundi hilo.
Wanajeshi wa Muungano wa Afrika wamekuwa wakiukaribia mji huo kwa miezi kadhaa sasa.

Wadadisi wanasema kuwa kwa kundi hilo kupoteza udhibiti wa Kismayo, itakuwa pigo kubwa kwao ingawa kundi hilo limesema litaendelea kupigana licha ya hilo kufanyika.

Mnamo mwezi Julai, ripoti ya Umoja wa mataifa, ilipiga marufuku biashara ya mkaa kutoka Kismayo hadi Merca . Biashara hiyo imesaidia Al-Shabaab kupata mamilioni ya dola licha ya baraza la usalama la umoja huo kupiga marufuku biashara ya mkaa kutoka Somalia.

Ripoti hiyo ilishutumu Saudi Arabia miongoni mwa nchi zingine kwa kutozingatia marufuku hiyo na kuendelea kununua mkaa kutoka Somalia.
CHANZO-BBC

Monday, September 17, 2012

JESHI LA POLISI LADAIWA KUPANGA MBINU CHAFU ZA KUMLINDA MTUHUMIWA WA MAUWAJI YA MWANGOSI

                                                Na Mwandishi wetu

IGP Said Mwema
Huku watanzania wakipinga hatua ya jeshi la polisi mkoa wa Iringa kumfikisha mahakamani mtuhumiwa mmoja pekee Kati ya askari zaidi ya 6 waliokuwa wakimpiga Marehemu Daudi Mwangosi kabla ya kuuwawa kwa bomu,zipo taarifa zilizovujishwa na askari mkoani Iringa kuwa imeandaliwa mbinu chafu ya kumtetea mtuhumiwa huyo ili kuonekana kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa na tatizo la utindio wa ubongo.

Mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com umedokezwa na mmoja Kati ya makachero wa polisi ambao wanapinga unyama huo wa mwanahabari Daudi MWANGOSI kuuwawa kwa bomu.

Imedaiwa kuwa lengo la kutaka kufanya hivyo ni kutaka kulilinda jeshi zima la polisi na waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Dkt Emmanuel NCHIMBI huku wengi wao wakihoji sababu ya Kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Iringa chini ya mwenyekiti wake mkuu wa mkoa wa Iringa Dkt Christine Ishengoma kuendelea kuwa Kimya hadi sasa.

Pamoja na kuhoji ukimya wa serikali ya mkoa wa Iringa pia ukimya wa Waziri mkuu na Rais Jakaya kikwete bila Kutoa rambi rambi Kama alivyozoeleka katika misiba mbali mbali ukiwemo wa msanii Kanumba na mingine huku Mauwaji haya Makubwa ambayo yameigusa tasni nzima ya habari hakuna aliyezungumzo chote chote.
CHANZO-Francisgodwin.blogspot.com

Wauwaji wa balozi wakamatwa Libya

Wauwaji wa balozi wakamatwa Libya

Na Mashirika ya habari
Libya
Mkuu wa bunge la Libya anasema kuwa watu kama 50 wamekamatwa kwa kuhusika na mauaji ya balozi wa Marekani mjini Benghazi juma lilopita.
MegaryefKiongozi wa Bonge Bw. Megaryef.

Mohammed Megaryef, kiongozi wa bunge, alisema hakuna shaka kuwa shambulio hilo lilikuwa limepangwa na siyo tu la kulipiza kisasi kwa filamu ya Marekani iliyokejeli Uislamu.
Akizungumza na shirika la habari la Canada, CBS, Bwana Megaryef alisema anaamini wageni wenye uhusiano na Al-Qaeda walihusika.
Balozi wa Marekani, Chris Stevens, na Wamarekani wengine watatu, waliuwawa wakati guruneti lilipopiga ubalozi mdogo wa Marekani mjini Benghazi na kuwaka moto.

JAPANI YAZIDI KUPINGWA VIKALI NCHINI CHINA

 Na Mashirika ya habari
China
Maandamano ya kuipinga Japani yameendelea katika miji kadha ya Uchina katika mzozo unaozidi kurindima  kuhusu visiwa vilioko katika bahari ya kusini ya Uchina.
Maandamano yaliyofanywa Uchina mbele ya ubalozi wa Japani Jumapili
Polisi walitumia gesi kutawanya watu waliokuwa na hasira kwenye mji wa Shenzhen, kusini mwa Uchina, huku waandamanaji wakichoma bendera za Japani katika mji wa jirani, Guangzhou.

Japan imetoa wito kwa Uchina kuhakikisha usalama wa raia wa Japani, huku Uchina imezidi kusisitiza madai yake ya visiwa hivo viitwavyo Senkaku au Diaoyu.

Kwa miaka mingi hayakutokea maandamano ya ghasia Uchina kama haya, kuipinga Japani.
Watu waliokuwa na hasira walichoma moto bendera ya Japani, walibeba mabiramu ya kuitusi Japani na kurusha mawe ubalozini.

Karakana na biashara za Japani pia zililengwa na waporaji na kuchomwa moto.
Hata hivo maandamano hayo hayakutajwa na vyombo vya habari vya taifa na juhudi zimefanywa kudhibiti majadiliano kwenye internet.

Sababu ni kuwa maandamano yenyewe ni mazuri kufikisha ujumbe kwa Japani, lakini yanaweza kugeuka na kuwa dhidi ya serikali piya.
Wakuu wa Uchina wanaamini kuwa Japani imevunja makubaliano ya namna fulani, kwamba hali ibaki kama ilivokuwa.
Serikali ya Japani inasema inavinunua visiwa hivo kutoka serikali ya mji wa Tokyo ili kuzuwia serikali ya jiji kufanya miradi na kujenga katika visiwa hivyo.
Lakini Uchina inaona hatua hiyo ni juhudi za kuthibitisha kuwa visiwa hivyo ni vya Japani.

Thursday, September 13, 2012

SERIKALI YATAKIWA KUBORESHA HUDUMA KATIKA HOSPITALI YA MISHENI PERAMIHO

Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Misheni  Peramiho Dkt Ansigar Stuffe

Na Joseph Mwambije
Peramiho
MKURUGENZI  Mkuu wa Hospitali ya Misheni peramiho  Mkoani Ruvuma  Dkt Ansigar Stufe ameiomba Serikali kuipasisha  Hospitali hiyo kuwa ya rufaa  kivitendo kwa kuboresha na kuongeza majengo na  Wafanyakazi ikiwemo  kuwalipa mishahara tofauti na ilivyo sasa inaitwa Hospitali ya rufaa kwa maneno tu.

Waziri mkuu wa zamani Misri afungwa jela


 Na Mashirika ya habari
Libya
Bw. Nazif Ahmed

 Na Mashirika ya habari
Libya
Bwana Nazif, ambaye alikuwa waziri mkuu kuanzia mwaka 2004 hadi mwaka jana wakati mapinduzi ya kiraia yalipofanyika, pia ameamrishwa kulipa faini ya dola milioni 1.5.
Mwaka jana Ahmed Nazif alifutwa kazi kwa muda wa mwaka mmoja baada ya kushtakiwa kwa kosa la kupata faida haramu kutokana na biashara alizofanya kinyume na sheria.
Nazif alikuwa mmoja wa maafisa wakuu katika serikali ya rais wa zamani Hosni Mubarak.
Alikamatwa miezi kadhaa baada ya kuacha kazi mwezi Januari mwaka 2011, muda mfupi kabla ya rais Mubarak kuachia ngazi.
Maafisa kadhaa wa uliokuwa utawala wa Mubarak wamefikishwa mahakamani kwa aidha kosa la njama ya kuwaua waandamanaji au makosa ya kuhusiana na ufisadi.
Mubarak alihukumiwa kifungo cha maisha jela mwezi Juni baada ya kuhusishwa na mauaji ya waandamanaji.
CHANZO-BBC

Wednesday, September 12, 2012

Balozi wa Marekani auawa Libya



Na Mashirika ya Habari
Libya
Balozi wa Marekani nchini Libya ameuawa baada ya kushambuliwa na watu waliokuwa wamejihami na kuvamia ubalozi wa Marekani Mashariki mwa mji wa Benghazi.           
Balozi J Christopher Stevens, ni miongoni mwa maafisa wengine wa ubalozi waliouawa kufuatia maandamano kuhusu filamu iliyotolewa nchini humo ikimkejeli Mtume Muhammad.

Idara ya mambo ya ndani nchini Marekani, imethibitisha tu kifo cha afisaa mmoja wa ubalozi huo ingawa bado haijataja jina lake.
Maandamano ya kupinga filamu hiyo pia yalifanyika mjini Cairo dhidi ya ubalozi wa Marekani.
Wakati huohuo, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bi. Hilary Clinton, amelaani mashambulizi hayo.
Serikali ya Libya imetaja shambulio hilo kama kitendo cha uoga.
Ubalozi huo uliteketezwa na watu waliojihami kwa bunduki kulalamikia filamu moja iliyotengenezewa nchini Marekani ambayo wanasema inamdhihaki Mtume Mohammed.
Wanamgambo hao wanaoripotiwa kuwa na ufungamano na kundi la waislamu wenye msimamo mkali walitumia maguruneti ya kurushwa kwa roketi kuvamia ubalozi huo kabla ya kuiteketeza. Maafisa wa Libya wameiambia BBC kwamba hali imetulia kwa sasa.
Machafuko hayo ya Libya yalijiri saa kadhaa baada ya maelfu ya waandamanaji kukusanyika nje ya ubalozi wa Marekani mjini Cairo kuelezea hasira zao kuhusu filamu hiyo kumhusu Mtume Mohammed.
Kwa wakati mmoja waandamanaji hao waliingia ndani ya ubalozi huo na kuichana bendera ya Marekani na kurejesha yao.

Tuesday, September 11, 2012

MATAIFA YA NJE YANATAKA KUTUPIGANISHA NA MALAWI-WAZEE

 Wazee wa Mkoa wa Ruvuma wakimsikiliza Waziri wa mambo ya nje Bw. Benard Membe.
 Wakimpigia makofi wakati akiingia
 Mkuu wa Wilaya ya Songea Bw. Joseph Mkilikiti(katikati) wakati wa kumsubiri Waziri huyo.
 Waziri huyo akizungumza kwenye mkutano huo kuhusu mgogoro wa Mpaka kati ya Tanzania na Malawi na kubainisha kuwa jitihada za usulushishi zimeshindwa hivyo huenda suala hilo likapelekwa kwenye Mahakama za Kimataifa kuamuliwa na kwamba Sheria za Kimataifa zinataka  Nchi zinazoleta Shauri kupeleka suala kwa wadau kabla ya kupelekwa huko na ndicho Tanzania inachokifanya sasa.
 Meme akiwazee hao.
 Membe akisoma ramani ya Ziwa Nyasa inayoonyesha kuwa Mpaka uko katikato ya Ziwa ambayo alipewa na Mzee Emanuel Chilokota mabaye alieleza kwa kina jinsi anavyoifahamu MBAMBA BAY.
 Bado akipitia  ramani hiyo
 Mzee Ally Jaibu akisisitiza kuwa Mpaka uko kati kati ya Ziwa na kwamba Mataifa ya Ulaya yanataka kuzigombanisha Nchi hizi mbili Tanzania na Malawi.
 Mzee Mustapha Njozi(85) ambaye alipigana Vita vya  pili vya dunia anasema kuwa aliwahi kuwauliza Waingereza wakati wa Vita vya pili ya dunia kwamba je itaweza kupiganwa vita nyingine kubwa ndani ya Afrika kama hiyo,wakamjibu kuwa haitapiganwa kwa Matakwa ya Afrika bali Nchi hizo za Ulaya zitaanzisha vita kutaka kuuza na kujaribu  silaha zao huku akisisisitiza kuwa mpaka uko kati kati ya Ziwa bali lengo kubwa ni hilo la Nchi hizo kugombanisha Nchi hizo mbili
 Naye Mzee Chilokota akisisitiza kuwa Mpaka uko kati kati ya ZIWA.
Membe akizungumza.kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Said Mwambungu

WANAHABARI RUVUMA KATIKA MKUTANO NA VIONGOZI WA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA

 Mwenyekiti wa Tume ya mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba akizungumza  na waandishi wa habari kwenye Hoteli ya Seedfarm Villa Mjini Songea kuhusu mikutano ya Tume hiyo katika Mkoa wa Ruvuma huku akiwataka wanawake kujitokeza kwa wingi kwenye mikutano kutoa maoni yao kwa kuwa wanaohudhuria ni wachache ukilinganisha na wanaume.
 Hapa akiwa na Mwenyekiti wa Kundi la 5  Profesa Mwesiga Beregu  wakiwasikiliza wanahabari
 Baadhi ya wanahabari wakisikiliza.
 Geofrey Nilahi wa Radio Maria  akizungumza kwenye mkutano huo.
 Alpius Mchucha akizungumza kuhusu ushiriki wa wanafunzi wa wa Shule za msingi kwenye mikutano hiyo.
 Nathan Mtega wa Gazeti la Nipashe akizungumza kwenye Mkutano huo.
 Andrew Chatwanga-Katibu wa Chama cha Waaandishi wa habari Mkoa wa Ruvuma akizungumza kwenye mkutano huo.kushoto ni Joyce Joliga wa gazeti la Mwananchi  songea.
 Mjumbe wa Tume ya mabadiliko ya Katiba A-Shaymaa Kwegyir akiwa kwenye mkutano huo.
 Mkuu wa Wilaya ya Songea Bw. Joseph Joseph Mkilikiti(kushoto) pamoja na mjuumbe wa tume hiyo toka Zanzibar Bw. Ally Sale

Wanahabari wakifuatila kwa makini ktk mkutano huo.

Harambee Ya Mjane Wa Daud Mwangosi; Michango Inakaribia Shilingi Milioni Tano

Harambee Ya Mjane Wa Daud Mwangosi; Michango Inakaribia Shilingi Milioni Tano

MAREHEMU DAUD MWANGOSI(ALIYESHIKA MAIKI AKIZUNGUMZA)ENZI YA UHAI WAKE.WA PILI KULIA NI RPC WA MKOA WA IRINGA MICHAEL KAMUHANDA,ANAYEFUATIA NI MKUU WA WILAYA YA IRINGA DKT  PRISCA WARIOBA

 Michango zaidi bado inaendelea kutolewa. na unaweza kutoa michango hiyo na kuikabidhi kwa mjane wa marehemu kama itakavyorekodiwa hapa. Hivyo, aliye  na dhamira ya kumsaidia mjane wa Marehemu bado anakaribishwa kutoa mchango wake.  Mwisho wa   kukusanya ni mwisho wa mwezi huu ( Septemba)

Unaweza kuchangia kwa kutumia; M-Mpesa, Tigo Pesa, Airtel Money au NMB Mobile. Kwa namba 0754 678 252, 0712 95 61 31, 0788 111 765 ( Kwa walio nje mnaweza kutuma kwa Western Union, jina la mpokeaji- Maggid Mjengwa,  Tafadhali nijulishe kama utatuma kwa njia ya Western Union )Background:Ndugu zangu,  Daud Mwangosi ambaye pia alikuwa ' Mwanakijiji' mwenzetu hapa  Mjengwablog hatunaye tena.Nimemfahamu Daud Mwangosi  tangu mwaka 2004 nilipofika Iringa. Tangu wakati huo, amekuwa akiinipa ushirikiano mkubwa kwenye kazi ya kutangaza shughuli za kijamii kwenye  Vyuo Vya Maendeleo ya Wananchi. Ni  kwa kupiga picha za televisheni na kurusha habari kwenda Channel Ten; Iwe ni kwenda naye Ilula au Njombe, Daud Mwangosi  alikuwa tayari kila nilipomwomba aongozane nami kwa shughuli ya kijamii.

Mara nyingi nilimkuta Daud ofisini kwake  ( Picha ya kwanza juu) akichapa kazi na   huku mkewe akimsaidia kazi nyingine. Daud Mwangosi alikuwa mbunifu. Alikuwa ni mwenye kiu ya kujifunza mambo mapya kwenye teknolojia ya habari na mawasiliano.

Najua Daud Mwangosi alikuwa na  malengo ya kuendeleza shughuli zake za ujasiriamali.  Mbali ya mambo mengine, alikuwa na Photocopy machine ya kumwongezea kipato  ambayo iliharibika mwaka jana. Akawa na ndoto ya kuwa na studio ndogo ya kupiga picha za vipande ( Passport Size). Yote ni katika kumwongezea kipato kutunza familia yake.

Leo Daud Mwangosi hayuko nasi. Ameacha familia, mjane  na watoto wanne;  Itika Mwangosi ( Mjane) Nehemia Mwangosi ( 17) Kidato cha Nne Malangali Sekondari, Hetzgovina Mwangosi  (12) Bathsheba Mwangosi (9) na Moria Mwangosi ( 2)Namini Daud Mwangosi angependa shughuli alizokuwa akizifanya ziendelee na zije kuwasaidia watoto wake pia.

Jana na leo nimewasiliana na mjane wa marehemu Mwangosi ambaye bado yuko Tukuyu. Nikamwambia kuna ' Wanakijiji ' wa Mjengwablog walioguswa na msiba wa Mwangosi na wangependa kutoa pole yao imsaidie katika kupata mwanzo kutoka hapa alipo sasa. Mjane wa Mwangosi amefarijika sana kusikia habari hizo.

Kwa vile tayari ameahidiwa msaada wa kusomeshewa watoto. Msaada anaouhitaji kwa sasa ni kupata photocopy machine ( Used)  na kodi ya pango la ofisi. Jumla yake kwa yote hayo mawili haitazidi shilingi za Kitanzania milioni mbili na laki mbili. Hivyo msaada anaouomba kwa wenye mapenzi mema ni shilingi 2, 200,000 ( Shilingi milioni mbili na laki mbili). Shughuli hizo zitamsaidia kujikimu.

Kutokana na hali aliyo nayo sasa, Mwenyekiti wenu napendekeza nichukue jukumu la kuratibu michango hiyo.  Shime tushirikiane kufanikisha hili ili tumsitiri mjane wa mwenzetu Daud Mwangosi. Napendekeza ifikapo mwisho wa mwezi huu  ( Septemba) tuwe tumefanikisha zoezi hili kwa yeyote aliye nacho, hata kama ni shilingi elfu tano, ni msaada mkubwa.

Mjengwablog bado tuna rekodi nzuri katika kuchangishana kuwasaidia  wenye kuhitaji. Itakumbukwa, huko nyuma,  kwa pamoja, tulifanikisha kukusanya michango ile ya watoto wa Somalia na kuikabidhi UNICEF, Dar es Salaam. Ni zaidi ya shilingi milioni mbili.Tulifanikisha mchango wa kusaidia ukarabati  wa maktaba ya Kijamii kijijini Mahango, Madibira. Zaidi ya shilingi milioni nne.Sasa ni zamu ya kumchangia mjane wa mwenzetu Daud Mwangosi. Kinachohitajika ni milioni mbili na laki mbili.Naam, kutoa ni moyo, usambe ni utajiri. Mwenyekiti wenu na familia yangu naanza kwa kuchangia shilingi laki moja.Na kama kawaida, taarifa za waliochanga na kiasi kilichopatikana kitawekwa kwenye blogu kwa kila mmoja kuona.

Namna ya kuwasilisha michango: Tumia M-Mpesa, Tigo Pesa, Airtel Money au NMB Mobile. Kwa namba 0754 678 252, 0712 95 61 31, 0788 111 765 ( Kwa walio nje mnaweza kutuma kwa Western Union, jina la mpokeaji- Maggid Mjengwa)

Natanguliza Shukrani.

JUMJLA YA MICHANGO HADI SASA NA WATOAJI WAKE:

1. Chris Cremence                                     100,0002. Anonymous                                             500,0003. Maggid Mjengwa                                     100,0004. Raymond Kasoyaga                                   20,0005.Edward Mgogo                                            10,0006.Joachim Kiula                                                5,0007.Libory Muhanga                                             5,0008.Geofrey Kagaruki                                        10,0009.Sadiki Mangesho                                         10,00010. Edwin Namnauka                                      40,00011.Daud Mbuba                                               10,000 12. Anonymous                                             200,00013.Mikidadi Waziri                                              6,00014. Bungaya Mayo                                             5,50015. Abraham Siyovelwa                                    50,00016. Godfrey Chongolo                                       22,22217. Jacob Mwamwene                                       51,00018. Denis Bwimbo                                        153,683 19. Zanzibar Ni Kwetu                                     150, 46420.Felex Mpozemenya                                       10,00021.Rweyendera Ngonge                                     11,00022. Festo Temu                                                      10,00023.  Azaria Mulinda                                                 10,00024.Khatibu Kolofete                                                   5,00025. John Bukuku                                                  25,00026. Abel                                                                10,00027. Hafidh Kido                                                     10,00028. George Mtandika                                            16,000 29. Shy-Rose Bhanji                                          200,00030. Raymond Nkya                                               52,00031. Maganga Sambo                                             10,00032. Felix Mwakyembe                                             10,00033. Abdul Diallo                                                         5,00034.  Newton Kyando                                              20,000 35. Galanos Myinga                                               20,00036. Anonymous ( 200 Euro)                                    497,000   37.   Yasinta Ngonyani                                              50,00038.  Prosper/ Willy  ( Japan)                                    314,00039.   Nuru Mkeremi                                                   131,00040. Anonymous                                                            50,00041.  Josephine Mahimbo                                              50,00042.  Anonymous                                                         150,00043. Heladius Macha                                                      30,00044. Emma Malele                                                           10,00045.  Anonymous                                                            60,00046. Hendry Mlay                                                            35,00047. Hosea Ngowi                                                            10,00048. Athuman Zuber                                                           5,00049. Hyancinth Komba                                                        7,50050. Edson Kihongole                                                       11,50051.  Godfrey Emmanuel                                                 20,50052.  Deus  M                                                                   27,00053.Sigisto Amon                                                              10,00054.Issa Kubonya                                                              10,00055. Richard Dalali                                                               6,00056.Fadhili Mtanga                                                            20,00057.  Polycarp Ngowi                                                            5,00058.  Salehe Mfaume                                                          10,00059. Deodatus Balile                                                           20,00060. Moses Ringo                                                                15,00061. Dr Rukoma                                                             100,000 62. Mobhare Matinyi                                                     100,00063. Humphrey Simba                                                       16,00064. Fredrick Kyambile                                                       10,00065.John Mwakyusa                                                            20,00066. Abdul Njaidi                                                                  40,00067. Fidelis Francis                                                               10,00068.Mutachumwa Mukandala                                                 10,00069. Augustino Lukosi                                                           12,50070. Goodluck Arobogast                                                       20,00071. Lusajo Mwasaga                                                             15,00072. Carolina Reynolds                                                              5,50073. Rugenamu Kawa                                                             30,00074. Innocent Kimario                                                                 5,00075.  Chadema UK                                                                1,000,000    

                                            Jumla:                                                   4,559,000   ( Milioni Nne Na Laki Tano Na Hamsini Na  Tisa Elfu)

HABARI HII NI KWA HISANI YA KWA HISANI YA  MTANDAO WA MJENGWA